SUMATRA KUHAKIKISHA BANDARI ZOTE HAPA NCHINI ZINATOA HUDUMA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA.
Mamlaka ya usafiri na
usafirishaji wa nchi kavu na majini nchini (SUMATRA) imesema, itahikisha kuwa Bandari zilizopo nchini zinatoa huduma kwa kiwango cha kimataifa ili ziweze
kushindana na bandari za nchi jirani ikiwa ni pamoja na kupewa leseni.
Akizungumza katika mkutano wa wadau wa Sekta ya usafiri
wa maji uliofanyika
Jijini Mwanza kuhusu utekelezaji wa kanuni za leseni za shughuli za bandari,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Gilliard Ngewe alieleza kuwa Sumatra kama
mdhibiti, imepewa jukumu la kuwezesha bandari zinatoa huduma bora na
zenye ufanisi.
Ngewe alieleza katika kuboresha utendaji na usimamizi wa shughuli
za bandari, serikali ilipitisha kanuni za leseni zinazofahamika kama
SUMATRA (Licencing of Port Terminal Operators) Regulations, 2011 ikiwa
ni moja ya Nyenzo inayotumiwa na mamlaka hiyo ili kufikia malengo yaliyo
kusudiwa.
“kuendelea kukua kwa biashara za kimataifa kunashinikiza bandari
zetu zilizopo katika ukanda wa bahari na katika maziwa yetu kulenga kutoa
huduma kwa viwngo vya juu.” alisema Ngewe.
Alisema tangu kuanzishwa kwa kanuni hizo mwaka 2011, utekelezaji
wake ulikuwa haujaanza kutokana na mamlaka kuona umuhimu wa kutoa elimu kwanza
ya kanuni kwa waendeshaji wa bandari, hali inayopelekea kupatikana kwa manufaa
yaliyo kusudiwa katika uboreshaji wa bandari.
Aliyataja manufaa hayo kuwa ni pamoja na kudhibiti
ulinzi wa nchi kwa kuhakikisha taratibu na sheria za nchi zinazingatiwa
ipasavyo hususani udhibiti wa watu, meli na bidhaa zinozo ingia na kutoka
nchini kupitia bandari hasa enzi hizi za kuongezeka kwa ughaidi na biashara
haramu za madawa ya kulevya.
Zingine ni kurahisisha utekelezaji wa sheria mbalimbali
za nchi zinazosimamiwa na idara na taasisi nyingine za serikali katika maeneo
hayo ikiwa ni pamoja na sheria ya Forodha, kanuni za afya Bandarini
ambazo zimelenga kudhibiti uambukizaji wa maradhi kutoka nchi moja hadi
nyingine.
Ngewe aliongeza kuwa, kwa upande wa kanda ya ziwa, ziwa viktoria
ni miongoni mwa maeneo yenye bandari nyingi zisizo rasmi(zisizo na leseni)
kutokana na hali hiyo, ni vema kukawepo na usimamizi imara ili kupwepo na
huduma bora na salama.
“sasa Sumatra imepanga kutekeleza kanuni hizi za leseni za
shughuli za bandari katika kipindi hiki cha kuanzia mwaka huu wa fedha
2014/2015” alisema.
Mwisho.
Na:Prisica Japhes.
No comments: