LIVE STREAM ADS

Header Ads

MADEREVA NYANZA BOTTLING COMPANY WAFUTA DHANA KWAMBA MAGARI YA KAMPUNI HIYO NI MABOVU.

Christopher Mwita Gachuma ambae ni Mkurugenzi wa Nyanza Bottling Company (Kushoto) akiwa na RK Bala ambae ni Mtendani Mkuu wa Kampuni hiyo.
Madereva wa Kampuni ya Nyanza Bottling iliyopo Mkoani Mwanza ambayo inajishughulisha na utengenezaji wa Vinywaji jamii ya Cocacola wamemshukuru Mkurugenzi wa Kampuni hiyo baada ya kuwaendeleza kimafunzo sanjari na Kuhakikisha kuwa Kampuni hiyo inakuwa na Magari yanayokidhi viwango katika shughuli zao.


Madereva hao waliyasema hayo jana jumamosi katika
hafla ya kusherehekea Jubilee ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Nyanza Bottling mwaka 1990, hafla ambayo ilifanyika Igoma Jijini Mwanza yalipo Makao Makuu ya Kampuni hiyo.

Akitoa shukrani za Madereva wa Kampuni hiyo, Peter Mafwele alibainisha kuwa ile dhana iliyokuwa imezagaa mtaani kwamba Madereva na Magari ya Cocacola ni mabovu imefutwa baada ya wao pamoja na Mataniboi wao kupatiwa mafunzo zaidi sanjari na kuboresha Ubora wa magari ya Cocacola.

Zaidi ya yote Walimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyanza Bottling kutokana na uongozi wake kujaa upendo na huruma sanjari na kuajiri wafanyakazi wake bila kujali rangi, kabila wala dini ya mtu ambapo Kampuni hiyo imesheheni watu wote kutoka Kusini, Kaskazini, Magharibi na Mashariki.

Akizungumza kwa niaba ya Wafanyakazi wote wa Wafanyakazi wote wa Nyanza Bottling katika hafla hiyo ya Miaka 25, Mashaka Kaguna ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TUCTA Tawi la Nyanza alibainisha kuwa kwa Mwaka 2014 wafanyakazi wa Kampuni hiyo walikumbana na changamoto kadhaa ambazo ni pamoja na Makato makubwa sanjari na kucheleweshewa malipo yao na hivyo kumuomba Mkurugenzi wa Kampuni hiyo kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa.

Kwa upande wa Wafanyakazi, Kaguna alibainisha kwamba watahakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kuwezesha Kampuni hiyo kuendelea kuongoza katika Ubora wa Gold (Dhahabu) ilionao.
Christopher Mwita Gachuma ambae ni Mkurugenzi wa Nyanza Bottling Company alibainisha kuwa changamoto na matatizo yote yaliyozungumzwa na Wafanyakazi wake yatafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

Awali RK Bala ambae ni Mtendaji Mkuu wa Nyanza Bottling Company aliwataka wafanyakazi wa Kampuni hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku wakizingatia nidhamu na Unyenyekevu katika Majukumu yao.

Sherehe hiyo iliambatana na burudani mbalimbali ambapo kundi la Vijana wa Mabatini Jijini Mwanza lilidondosha bonge la burudani kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Nyanza Bottling pamoja na Wageni waalikwa jambo lililonogesha sherehe hiyo zaidi.

Kila Mwaka Gachuma huwakutanisha Wafanyakazi wa Makampuni yake yote yaliyo chini ya CMG Group kwa ajili ya Kusherehekea kwa pamoja ambapo Mwaka huu sherehe hiyo imeambatana na jubilee ya Miaka 25 ya Nyanza Bottling Company.
Viongozi, Watendaji na Wafanyakazi mbalimbali wa Nyanza Bottling Company wakiongozwa na Mkurugenzi wake Christopher Mwita Gachuma (Wa Kwanza Kushoto).
Viongozi, Watendaji na Wafanyakazi mbalimbali wa Nyanza Bottling Company wakiongozwa na Mkurugenzi wake Christopher Mwita Gachuma (Wa Kwanza Kushoto).
Viongozi, Watendaji na Wafanyakazi mbalimbali wa Nyanza Bottling Company.
Viongozi, Watendaji na Wafanyakazi mbalimbali wa Nyanza Bottling Company.
Viongozi, Watendaji na Wafanyakazi mbalimbali wa Nyanza Bottling Company.
Wafanyakazi wa Idara mbalimbali kutoka Nyanza Bottling Campany.
Wafanyakazi wa Idara mbalimbali kutoka Nyanza Bottling Campany.
Wafanyakazi wa Idara mbalimbali kutoka Nyanza Bottling Campany.
Wafanyakazi wa Idara mbalimbali kutoka Nyanza Bottling Campany.
Wafanyakazi wa Radio Metro Fm Jiji Mwanza, Kushto ni Alphonce Tonny Kapela, katikati ni Alex Ngusa na kulia ni Loyce Nhaluke aka Mamaa Lonah.
Wafanyakazi wa Radio Metro Fm Jiji Mwanza, Kushto ni Alphonce Tonny Kapela, katikati ni Alex Ngusa na kulia ni George Binagi-GB Pazzo. (Mmiliki pia wa Mtandao huu).
Mashaka Kaguna ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi nchini TUCTA Tawi la Nyanza akitoa salamu za Wafanyakazi wa Nyanza Bottling Company.
Peter Mafwele akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi wa Nyanza Bottling Company kwa niaba ya Madereva wa Kampuni hiyo.
Peter Mafwele (Kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Nyanza Bottling Company Christopher Mwita Gachuma (Kulia) salamu zao za Shukrani.
Marco Masaka ambae ni Mkuu wa Masoko Nyanza Bottling Company.
Kushoto ni RK Bala ambae ni Mtendaji Mkuu Nyanza Bottling Company akiwa na Marco Masaka ambae ni Mkuu wa Masoko katika Kampuni hiyo.
Watendaji wa Idara mbalimbali kutoka Nyanza Bottling Company wakitambulishwa na RK Bala (wa pili kushoto) ambae ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo kutokana na mchango wao katika Kampuni.
Watendaji wa Idara mbalimbali kutoka Nyanza Bottling Company wakitambulishwa na RK Bala (wa kwanza kushoto) ambae ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo kutokana na mchango wao katika Kampuni.
Christopher Mwita Gachuma ambae ni Mkurugenzi wa Nyanza Bottling Company (Kulia) akizungumza na wafanyakazi wake.
Christopher Mwita Gachuma ambae ni Mkurugenzi wa Nyanza Bottling Company (Kushoto) akiwabidhi watendaji wa Nyanza Bottling Company kwa niaba ya Wafanyakazi wengine kitabu kinachoelezea masuala mbalimbali kuhusiana na Kampuni hiyo.
Christopher Mwita Gachuma ambae ni Mkurugenzi wa Nyanza Bottling Company akizungumza na wafanyakazi wake.
Wafanyakazi mbalimbali wa Nyanza Bottling Company wakigonga Cheers Meza kuu.
Misosi Time sasa.
Pakua kadri uwezavyo.
Nyama za Kuku ziko poa sana.
Weka hicho kipande huku.
Hatimae Christopher Mwita Gachuma (Katikati) ambae ni Mkurugenzi wa Nyanza Bottling Company akafungua Disco na the Watu wakaanza kudance.
Mara watu wakaanza kujibwaga Uwanjani na hatimae disco likanoga kweli kweli.
Watoa burudani kundi kutoka Mabatini nao walitoa burudani nzuri kiasi cha kuwafanya kutuzwa ile mbaya.
Show Ikiendelea kama kawiz.
Hawa jamaa wanadance BALAAA...THE PIPOOO WALIINJOIII SAAANA!
TUPIGIE KUPITIA 0757 43 26 94 ILI KUWEKA SHUGHULI YAKO KATIKA MTANDAO HUU UNAOPENDWA KOTE DUNIANI KWA GHARAMA NAFUU KABISA.

No comments:

Powered by Blogger.