LIVE STREAM ADS

Header Ads

OJADACT YAONGEA NA WANAHABARI BAADA YA PROFESA MUHONGO KUJIUZULU.

Viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uharifu nchini Tanzania.
NDUGU WAANDISHI WA HABARI    KWANZA  TUNAWAPONGEZA  KWA KUCHUKUA NAFASI HII  KUJA KWETU  KUJUA  NINI  MTAZAMO WETU  BAADA YA  WAZIRI WA NISHATI  NA MADINI  SOSPETER  MUHONGO KUJIUZULU.

KATIKA KUJIBU  SWALI  LENU KUWA  "CHAMA  CHETU  KINATOA  MAONI  GANI BAADA  YA   PROFESSA  MUHONGO  KUJIUZULU"?

SISI  KAMA CHAMA
TUNAPONGEZA  UAMUZI  HUO  KWA KUWA   AMEWATENDEA  HAKI  WATANZANIA  KWA KUAMUA  KUJITOA  MWENYEWE  KATIKA UTEUZI WA   MH. RAIS  KWA MUJIBU WA IBARA  YA  36  YA  KATIKA.

NDUGU WAANDISHI  IKUMBUKWE  KUWA  CHAMA  CHA  WAANDISHI WA HABARI WA KUPIGA  VITA  MATUMIZI  YA DAWA  ZA KULEVYA  NA UHALI  TANZANIA (OJADACT) TULIKUWA  MSTARI WA MBELE  KUSHINIKIZA  WALE  WOTE  WALIOTAJWA KUHUSIKA KATIKA   UFISADI WA  AKAUNTI  YA  TEGETA ESCROW  WAJIVUE  AU  WAVULIWE  NYADHIFA  ZAO  NA MHESHIMIWA  RAIS  AU  KUJIVUA  WENYEWE   KWA MUJIBU WA KATIBA   NA SHERIA  NYINGINE  ZA  NCHI, TULIFANYA  PRESS  CONFERENCE  NANYI     DISEMBA 2  NA PIA  DISEMBA 31 MWAKA JANA.

DISEMBA  2, 2014  TULIMTAKA  MH. RAIS  AWAWAJIBISHE   AU  WAJIWABIBISHE  WENYEWE   WAZIRI WA NYUMBA NA MAKAZI  PROF  ANNA  TIBAIJUKA, WAZIRI WA NISHATI  NA MADINI PROF.  SOSPETER   MUHONGO, MWANASHERIA  MKUU  JAJI  FREDRICK WEREMA,  NA KATIBU MKUU WA  WIZARA  YA  NISHATI  NA MADINI   ELIAKIM  MASWI.

HADI  KUFIKIA   DISEMBA  31, SIKU  TULIYOKUTANA  NANYI  TENA  KWENYE  PRESS  CONFERENCE   KATI  YA  HAO  TULIOWATAJA  ALIKUWA  AMEBAKI  WAZIRI  MUHONGO  NA   SIKU  HIYO  TULIMSHINIKIZA  MUHONGO   KUKAA  PEMBENI  KWA HIARI  YAKE  NA   KAMA  ATASHINDWA  KUFANYA  HIVYO   BASI   TULIMTAKA    RAIS  JAKAYA MRISHO  KIKWETE   KUMWONDOA  KWA KUFUTA  UTEUZI  WAKE  NA  KUTEUA WAZIRI  MWINGINE

HIVYO    PRESH   ZETU   ZILIKUWA NA  SABABU ZA KIMSINGI   HASA  KUTETEA   UVUNJWAJI WA   SHERIA  ZA  NCHI   NA  KUWEKA  MASLAHI YA  TAIFA  MBELE.

HIVYO  BASI  TUNAMPONGEZA   KWANZA  SOSPETER MUHONGO     ANGALAU    KWA KUCHUKUA  MAAMUZI  HAYO  YA KUKAA  PEMBENI  ILI  KUWATENDEA   HAKI WATANZANIA  KWA MUJIBU WA  DHANA  YA  UWAJIBIKAJI WA   WAZIRI  MMOJA  MMOJA  KWA KUAMUA  KUJIHUDHURU, LAKINI  PIA  DHANA  YA  UTAWALA  BORA.

MSIMAMO  WETU  KAMA  CHAMA

CHAMA  CHETU NI WAUMINI WA  KUPIGA  VITA UHALIFU   HIVYO  BASI   TUNAWATAKA  WOTE  WALIOHUSISHWA NA  UFISADI WA  FEDHA  ZA  ECROW  AKAUNTI  BAADA   YA  KUJIHUDHURU WACHUKULIWE  HATUA  KALI  ZIKIWEMO  ZA KUFIKISWA  MAHAKAMANI  NA  KUFILISIWA    MALI ZAO  KWA MUJIBU WA SHERIA   ZA NCHI  ILI  IWE  FUNZO  KWA  VIONGOZI  WENGINE  WANAOFISADI   RASIRIMALI  ZA   TAIFA  NA KUWAACHA WATANZANIA  WENGINE  WAKIISHI   KAMA  WATUMWA  HUKU WAO  WAKIISHI KAMA  WAFALME.

Edwin Soko
Mwenyeki  OJADACT

No comments:

Powered by Blogger.