LIVE STREAM ADS

Header Ads

YAMETIMIA. CC YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM YAJAA PONGEZI HUKO ZANZIBAR.

Kamati Kuu ya CCM iliyoketi jana Kisiwandui, Zanzibar ilitawaliwa na pongezi pamoja na maagizo ya hapa na pale ya kichama. Taarifa za kuaminika toka ndani ya kikao husika zimeeleza kuwa CC imepitisha
karibu maazimio yote ya Kamati ya Komredi Mangula.
CC imepongeza ushindi kwenye Serikali za Mitaa. Pia CC imeipongeza Kamati Maalum ya Maadili chini ya Komredi Mangula kwa kuwabana na kuwarekebisha wagombea watarajiwa wa Urais.
"Hapo CC imesifu na kupongeza mwenendo wa wahusika kwasasa na kuwaona wanaofuata taratibu za chama. Hakukuwa na mjadala mkali kama ilivyotarajiwa" kilisema chanzo hicho toka Kisiwandui.
CC pia imempongeza na kumpa baraka Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa jinsi anavyoendelea kulishughulikia kwa weledi sakata la Escrow. Mwenyekiti ameahidi kuwa makini na mtenda haki katika hilo.
CC imeiagiza Sekretarieti ya CCM kufanya maandalizi kabambe ya Kura ya Maoni na uchaguzi mkuu kwa kutoa Ripoti mara kwa mara juu ya mikakati inayoendelea. Sekretarieti imeruhusiwa kuunda kamati mbalimbali za wataalamu ili kufanikisha maandalizi hayo.

CC imetambua na kupongeza ziara za kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa Ilani zilizofanywa na Sekretarieti chini ya Katibu Mkuu Kinana. "Hayo ndiyo makubwa humo. Kikao hakikuwa na mjadala mkalí. Kilitawaliwa na busara" kimesema chanzo cha taarifa hii.
Na: Mwandishi Wetu.

No comments:

Powered by Blogger.