LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMATI ZA MACHINGA MWANZA ZASIMIKWA RASMI. MWENYEKITI AWAONYA WATAKAOTUMIKA VIBAYA.

Baadhi ya Wanachama wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza.
Viongozi wa Kamati mbalimbali ndani ya Umoja wa Machinga Mkoa wa Mwanza, wamesimikwa rasmi kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa majukumu yao, huku mwenyekiti wa Muungano huo akitoa onyo kali kuwa wale wote watakaoshindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo watapoteza nafasi zao za uongozi ndani ya Umoja huo.

Akizungumza jana katika Ukumbi uliopo Florida Pub Jijini Mwanza wakati wa zoezi la kuwasimika viongozi na wajumbe wa Kamati zilizochaguliwa hivi karibuni, Said Tembo ambae ni Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoani Mwanza alibainisha kuwa jukumu kubwa la viongozi na wajumbe waliochaguliwa katika kuziongoza Kamati za Muungano huo ni kutetea maslahi ya Machinga Mkoa wa Mwanza na si vinginezo ambapo alionya kuwa watakaobainikaa kutumika vibaya ndani ya Muungano huo watachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kunyang'anywa nafasi zao za uongozi.

Katika hatua nyingine Tembo alitoa rai kwa Machinga Mkoa wa Mwanza kutoa ushirikiano wao kwa viongozi waliowachaguwa kwa lengo la kuhakikisha kwamba machinga Mkoa wa Mwanza wanatekeleza shughuli zao vyema bila kubugudhiwa huku akihitimisha hotuba yake kwa kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mageza Mulongo kwa kushirikiana na viongozi wengine wa Jiji la Mwanza ambao ni pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kwa kuruhusu Machinga waliokuwa eneo la Msikitini Makoroboi kuhamia eneo la Tanganyika Bus.

Kwa upande wake Mbogo Sabaganga Lubambi ambae ni Mlezi wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza, aliwasihi machinga wote kuwa watulivu ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu za kiuongozi katika kutatua changamoto mbalimbali pindindi zinajitokeza ili kuondoa dhana kwamba machinga ni watu wenye vurugu huku akiwahakikisha Machinga Jijini Mwanza kwamba atashirikiana nao bega kwa bega ili kuhakikisha kuwa kila Machinga anapata fursa ya kufanya shughuli zake bila adha yoyote.

Miongoni Mwa viongozi wa Kamati waliosimikwa jana ni pamoja na Hussein John ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi, Severian Sebastian ambae ni Mwenyekiti Kamati ya Afya na Mazingira, Dotto Shaban ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa sanjari na Fikiri Bugi Bugi ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo.
Endelea kutazama picha ili uweze kuona majina ya Viongozi na wajumbe wengine wa Kamati hizo.
Machinga Mkoa wa Mwanza.
Machinga.
Machinga
Machinga
Machinga
Mmoja wa Viongozi wa Kamati za Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza (Kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Muungano huo (Kushoto).
Manka Kassa (Kulia) ambae ni Katibu wa Kamati ya Afya na Mazingira akisalimiana na Said Tembo (Kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza.
Machinga.
Said Tembo ambae ni Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoani Mwanza.
Mbogo Sabaganga Lubambi ambae ni Mlezi wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza (Mwenye Kinasa sauti).
Mbogo Sabaganga Lubambi ambae ni Mlezi wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza.
Majina yote ya Viongozi waliosimikwa rasmi jana kwa ajili ya kusimamia Kamati za Ungozi ndani ya Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza.
Majina yote ya Viongozi waliosimikwa rasmi jana kwa ajili ya kusimamia Kamati za Ungozi ndani ya Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza.
Na: George Binadi-GB Pazzo

No comments:

Powered by Blogger.