AIRTEL YATOSHA ZAIDI, WASHINDI WATATU WAJISHINDIA MAGARI. BADO KUNA MAGARI 57. JIUNGE SASA.
Watanzania
na Watumiaji wa Mtandao wa Simu wa Airtel wamehimizwa kuendelea kutumia
vifurushi vya Airtel Yatosha Zaidi, ili kuingia katika droo ya kujishindia zawadi
nono ya Gari aina ya IST.
Jane Matinde ambae ni Afisa Mahusiano Airtel Tanzania aliyasema hayo jana Jijini Mwanza, wakati akizungumza na Wanahabari kuhusiana na Promosheni
hiyo ya Aitel Yatosha Zaidi ambayo inawawezesha watumiaji wa vifurushi vya
Airtel Yatosha Zaidi pia kujipatia vifurushi vya Internet, SMS na dakika za
kupiga kwenda mitandao yote ambapo vifurushi hivyo ni Vifurushi vya Siku, Wiki
pamoja na Mwezi.
Alisema Promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi inamwezesha mtumiaji wa
vifurushi vya Yatosha Zaidi hatimae kujishindia gari aina ya IST ambalo tayari
limelipiwa kila kitu, ambapo kila siku mshindi mmoja atakuwa akipatikana huku
promosheni hiyo ikidumu kwa muda wa siku 60 hivyo washindi 60 kila mmoja
ataweza kujishindia gari ambapo unachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# ili
kuweza kujiunga.
Baada ya Promosheni hiyo kuzinduliwa jumatatu ya wiki iliyopita,
tayari watumiaji watatu wa Mtandao wa Simu wa Aitel wamejishindia Gari aina ya
IST kila mmoja kupitia promoshoni hiyo ya Airtel Yatosha Zaidi inayoendeshwa na
Kampuni ya Airtel Tanzania. Bado kuna magari 57 ya kushindaniwa ambapo kuna jumla ya magari ya 60 yatatolewa kwa washindi.
Washindi hao
ni Namtapika Seif Kilumba (60) ambae ni mwalimu mstaafu kutoka Mkoani Mtwara,
Ramadhan Mohamed Dilunga (53) mkulima kutoka Kimanzichana Mkoani Pwani pamoja
na Mwajabu Omari Churian (27) ambae ni Mfanyabiashara kutoka Mbagala Jijini Dar es salaam ambao wote
waliibuka washindi na kujishindia gari
aina ya Toyota IST kila mmoja.
Emmanuel Raphael ambae ni Afisa Masoko Airtel Kanda ya
Ziwa alibainisha kwamba tayari gari
zinazoshindaniwa katika Promosheni hiyo ziko Jijini Mwanza na siku ya leo gari
hizo aina ya IST zitakuwa zikizunguka katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza
ambapo wateja wa Airtel watapata fursa ya kupiga picha katika magari hayo huku
wakipata huduma mbalimbali za Airtel.
Nae Rebecca
Mauma ambe ni Afisa Masoko Airtel Tanzania aliwakumbusha wateja na watumiaji wa
Airtel kuwa pindi mshindi wa Promosheni ya Yatosha Zaidi anapopatikana
anapigiwa simu kwa nambari 0684 29 11 05 hivyo wawe makini na baadhi ya watu
wenye nia mbaya ambao wanaweza kutumia fursa hii kwa njia ya utapeli.
Wanahabari/ Watangazaji Radio Free Africa. |
Wanahabari na Wadau wa Airtel. |
Wanahabari/ Watangazaji Radio Metro Fm. |
Wanahabari/ Watangazaji Radio Free Africa Kiss Fm. |
No comments: