MIDAHALO YA KUPANGA VIPAUMBELE VYA KUONGOZA MIJADALA YA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA MKOANI MWANZA.
Taasisi ya Mafunzo ya Biashara na Mawasiliano Africa Mashariki EABMTI (East Africa Busness and Media Trainining Institute) kwa Kushirikiana na Taasisi ya Twaweza, inatarajia
kuendesha Midahalo Mkoani Mwanza ikiwa na lengo la Kuibua vipaumbele vya Kimkoa vitakavyosaidia katika
kuongoza Mijadala ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu hapa nchini.
Rosemary Mwakitwange ambae ni
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi hiyo na
Mwongoza Midahalo hiyo aliyasema hayo hii leo Jijini Mwanza, wakati akizungumza
na Wanahabari juu ya Midahalo hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza.
Mwakitwange alibainisha kwamba katika Mkoa wa Mwanza itafanyika
Midahalo miwili ikiwa ni katika Wilaya ya Nyamagana pamoja na Ilemela ambapo
katika Midahalo hiyo, wazungumzaji wakuu wanatarajiwa kuwa ni pamoja na
Wakurugenzi, Mameya, Vyama vya Siasa vyenye Uwakilishi bungeni, Wabunge,
Madiwani, Asasi za Kiraia sanjari na Chama cha Wafanyabiashara hapa nchini
TCCIA.
Alisema katika Wilaya ya Nyamagana, Mdahalo utafanyika katika Ukumbi uliopo Gold Crest Hotel Ijumaa ya Wiki hii ambapo itakuwa ni February 06, 2015 ambapo katika Wilaya ya Ilemela Mdahalo utafanyika Jumamosi ya February 07, 2015.
Alisema lengo la Midahalo hiyo ni kutoa fursa kwa Wananchi,
Serikali na Wawakilishi wa Wananchi kujadili kwa pamoja na kutambua changamoto
zilizopo, ili kuepuka kuwa wasindikizaji katika mijadala mbalimbali ya Kitaifa
ambayo inatarajiwa kufanyika kupitia kwenye vyombo vya habari katika kuelekea
kwenye Uchaguzi Mkuu hapa nchini.
Katika
kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Octoba mwaka huu hapa
nchini, Taasisi ya Mafunzo ya Biashara na Mawasiliano Africa Mashariki EABMTI (East Africa Busness and Media Trainining Institute) kwa Kushirikiana na Taasisi ya Twaweza
kimeandaa Midahalo ya TANZANIA TUNAYOITAKA ambayo itakuwa ikirushwa katika kituo
cha Runinga cha ITV hivyo Midahalo inayofanyika hivi sasa Mikoani imelenga kuibua
vipaumbele vitakavyoongoza Mijadala katika Vipindi vya Midahalo ya TANZANIA
TUNAYOITAKA.
Rosemary Mwakitwange ambae ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mafunzo ya Biashara na Mawasiliano Africa Mashariki EABMTI (East Africa Busness and Media Trainining Institute). |
No comments: