LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAOMBWA KUWEKA KINGO ZA MTO MIRONGO JIJINI MWANZA ILI KUONDOA HATARI ILIYOPO.

Sehemu ya Kingo za Mto Mirongo mita chache kutoka Mtaa wa Liberty Jijini Mwanza ambazo zimeangushwa na Maji ya Mto huo kutokana na Mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa mwaka jana Jijini Mwanza.
Wafanyabiashara na Watumiaji wa daraja la Mto Mirongo lililopo Mita chache kutoka Mtaa maarufu wa Kibiashara wa Libert Jijini Mwanza, wameomba kufanyika kwa Ukarabati wa Kingo za Mto huo baada ya kusombwa na Maji kutokana na Mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa mwaka jana Jijini Mwanza.

Wakizungumza na Mtanzaniamedia Blog hii leo, Wafanyabiashara na Wananchi hao walisema kuwa
kukosekana kwa kingo katika Mto huo kunaleta hatari kwa watumiaji wa daraja hilo hususani watoto.

Kutokana na hali hiyo, Waliomba wahusika kuhakikisha kwamba wanafanya ukarabati katika daraja hilo kwa kuwa awali daraja hilo lilikuwa na Kingo za vyuma, lakini kingo hizo zilianguka hivi karibuni baada ya kushindwa kuhimili kasi ya maji yaliyokuwa yanapita katika mto huo kufuatia mvua kubwa ziliyonyesha Jijini Mwanza Mwishoni mwa Mwaka jana na kusababisha athari mbalimbali kwa wananchi.

"Sisi tunaotumia daraja hili hatufurahishwi hata kidogo na ukosefu wa kingo katika daraja hili hivyo tunaomba halmashauri ya Jiji la Mwanza kuangalia namna ya kufanya ili kutunusuru na majanga yanayoweza kutokea wakati wowote katika eneo hili hususani kwa watoto ambao mara nyingi nao hutumia daraja hili". Walisema Wafanyabiashara na Watumiaji wa daraja hilo la Mto Mirongo ambalo humwaga maji yake Ziwa Victoria Jijini Mwanza.
Sehemu ya Kingo za Mto Mirongo mita chache kutoka Mtaa wa Liberty Jijini Mwanza ambazo zimesalia baada ya nusu ya Kingo hizo kuangushwa na Maji ya Mto huo kutokana na Mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa mwaka jana Jijini Mwanza.
Na: George Binagi-GB Pazzo.

No comments:

Powered by Blogger.