WANANCHI WILAYANI ILEMELA MKOA WA MWANZA WALIA NA ILEMELA WANAYOITAKA.
Wananchi Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza
wameilalamikia Ilemela walioyonayo hivi sasa kutokana na kuwa katika hali mbaya
Kimaendeleo, ambapo wamebainisha kuwa wakati umefika wa Kuwa na Ilemela yenye
Maendeleo.
Wameyasema hao
jumamosi iliyopita katika Mdahalo wa Tanzania Tuitakayo ulioratibiwa na Taasisi
ya Mafunzo ya Biashara na Mawasiliano Africa Mashariki EABMTI (East Africa
Busness and Media Trainining Institute) kwa Kushirikiana na Taasisi ya Twaweza
uliokuwa na lengo la Kuibua vipaumbele vya Kimkoa vitakavyosaidia katika
kuongoza Mijadala ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika hapa
nchini mwaka huu.
Wananchi hao
walisema kuwa wangependa kuiona Ilemela yenye vipaumbele kadhaa vya kimaendeleo
ambavyo ni pamoja na upatikanaji wa elimu bora ambapo katika suala la elimu
walisema kuwa bado kuna idadi kubwa ya watoto ambao hawajapata fursa ya
kuandikishwa kuanza masomo yao sanjari na kuwa na wananchi wengi wasiojua
kusoma na kuandika.
Pia walieleza
kuwa sehemu kubwa ya wilaya ya Ilemela bado ni vijiji kulinganisha na Wilaya
jirani ya Nyamagana huku ikiwa inakabiriwa na ubovu wa miundominu ambayo
walisema kuwa ni mibovu kuliko Wilaya yoyote ile hapa nchini huku wakiongeza
kuwa bado Ilemela ina siasa chachu ambazo ni za chuki na zinapaswa kutokomezwa.
Aidha walisema
kuwa kuwa Wilaya ya Ilemela bado iko ICU (iko katika hali mbaya) katika suala
la huduma za Afya ambapo walilalamikia uhaba wa vituo vya Afya na Zahanati
katika Kata nyingi za Wilaya ya Ilemela sanjari na Ukosefu wa Hospitali ya
Wilaya huku wakishangazwa na kuwepo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ambae walihoji
juu ya uwepo wake.
Ili kuipata
Ilemela na Mwanza wanayoitaka Wananchi hayo walipendekeza wananchi kuchukua
hatua kwa kubadili mfumo wa Uongozi walionao na kuwachagua viongozi ambayo
watashirikiana na wananchi katika kuibadili sura ya Ilemela na hatimae kuwa na
Ilemela Waitakayo yenye maendeleo.
Akizungumza
katika Mdahalo huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Viola
Mbalikle aliahidi kuyafikisha kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo yale yote
yaliyozungumza na wananchi kwa lengo la kufanyiwa kazi.
Katika Mkoa wa
Mwanza ilifanyika Midahalo miwili ambapo katika Wilaya ya Nyamagana, Mdahalo
ulifanyika katika Ukumbi uliopo Gold Crest Hotel siku ya Ijumaa ya wiki
iliyopita ambapo ilikuwa ni February 06, 2015 na katika Wilaya ya Ilemela
Mdahalo ulifanyika Jumamosi ya February 07, 2015.
Rosemary
Mwakitwange ambae ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi hiyo na Mwongoza Midahalo
hiyo alisema kuwa lengo la Midahalo hiyo ni kutoa fursa kwa Wananchi, Serikali
na Wawakilishi wa Wananchi kujadili kwa pamoja na kutambua changamoto zilizopo,
ili kuepuka kuwa wasindikizaji katika mijadala mbalimbali ya Kitaifa ambayo
inatarajiwa kufanyika hivi karibuni ikiwa ni katika kuelekea kwenye kampeni za
Uchaguzi Mkuu hapa nchini.
Na:George Binagi-GB Pazzo
No comments: