LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YATAKIWA KUWACHUKULIA HATUA KALI ZA KISHERIA WATENDAJI WAKE.

Wananchi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza wakiuaga Mwili wa Magata Edson anaedaiwa kuuawa kwa kupigwa na polisi.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza kimeitaka Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya watendaji wake wakiwemo polisi wanaotenda kazi kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na kukiukaji wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu, wakati wa kuuaga mwili wa Kijana Magata Edson (25) mkazi wa Line Polisi mjini Misungwi Mkoani Mwanza anaedaiwa kuuawa kwa kupigwa na polisi Wilayani humo

Mtaturu ambae yuko Wilayani Misungwi kwa ziara ya siku mbili ambayo ilianza jana, alisema kuwa baadhi ya watendaji wakiwemo polisi wanaofanya mambo kinyumbe na haki za binadamu wachukuliwe hatua kwani hawana sababu za kuendelea kuwa ofisini.

“Niombe sana kufikisha ujumbe kwa IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini) Kwa niaba ya chama cha mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, tunaomba wale wote waliohusika kwenye jambo hili baya wachukuliwe hatua, hakuna sababu ya kufanyika uchunguzi wa kina kwa jambo hili kwani liko wazi” Alisema Mtaturu huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliokuwa wamefurika katika msiba wa kijana huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema BAVICHA Paschal Katambi Patrobas alisema kuwa jukumu la vyombo vya ulinzi hapa nchini ni kulinda usalama wa raia na mali zao hivyo vyombo hivyo vinapaswa kuhakikisha kuwa haki inatendeka badala ya kutenda udharimu kwa wananchi.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, vyama vya siasa pamoja na wananchi walihudhuria Mazishi ya Magata Edsoni ambae pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Vijana mtaa wa Line Polisi Mjini Misungwi aliefariki dunia March 23 mwaka huu.

Mazishi hayo yalifanyika jana katika Makaburi ya AIC Misungwi ambapo Marehemu ameacha mjane na mtoto mmoja. Binagi Media Group haikufanikiwa kumpata kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza ili kuzungumzia tukio hilo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye kofia) akisalimiana na Viongozi wa Chama hicho baada ya kuwasili Wilayani Misungwi jana kwa ajili ya ziara ya siku mbili inayohitimishwa hii leo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye kofia) akisalimiana na baadhi Viongozi wa Chama hicho baada ya kuwasili Wilayani Misungwi jana kwa ajili ya ziara ya siku mbili inayohitimishwa hii leo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (katikati mwenye kofia) akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za chama hicho Wilayani Misungwi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akisalimiana na baadhi ya waombolezaji waliofika kuhani msiba wa Magata Edson nyumbani kwao Line Polisi Misungwi.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza wakitoa salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Magata Edson aliefariki hivi karibuni.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akitoa salamu za pole katika Msiba wa Magata Edson.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba wa Magata Edson.
Jeneza alilopumzishwa kijana Magata Edson (25) Mkazi wa Line Polisi Misungwi Mkoani Mwanza.
BINAGI MEDIA GROUP; PUMZIKA KWA AMANI MAGATA EDSON.
CHANZO:METRO FM

No comments:

Powered by Blogger.