LIVE STREAM ADS

Header Ads

FARAJA NYALANDU ASEMA KILA MMOJA ANA WAJIBU WA KUMTETEA MWANAMKE. MSIKILIZE ZAIDI HAPA.

NA:JOEL MADUKA
WANANCHI WAMETAKIWA KUTAMBUA KWAMBA KILA MMOJA KATIKA JAMII ANA WAJIBU WA KUHAKIKISHA KUWA ANAMTETEA MWANAMKE NA KUMLNDA DHIDI YA UNYANYASAJIA AMBAO UMEKUWA UKIJITOKEZA KATIKA JAMII.

HAYO YALISEMWA JUZI JUMAPILI NA FARAJA LAZARO NYALANDU AMBAE NI MKE WA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KATIKA  SIKU YA MWANAMKE DUNANI ILIYOANDALIWA NA WANAFUNZI WA KIKE WA CHUO CHA ST.AUGUSTINE KILICHOPO JIJINI MWANZA.

NYALANDU AMBAE ALIKUWA MISS TANZANIA MWAKA 2004, ALISEMA KUWA KILA MTANZANIA MWENYE MAPENZI MEMA NA MWANAMKE ANATAKIWA KUHAKIKISHA KUWA ANAKUWA TAYARI KWA KUMLINDA MWANAMKE, IKIWA NI PAMOJA KUTOKOMEZA SUALA ZIMA LA UKEKETAJI NA PIA MASWALA YA UTAKASO AMBAYO NI MILA POTOFU ZINAZOENDELEA KUMKANDAMIZA MWANAMKE.

AKISOMA RISALA KWA MGENI RASIMI,  MAKAMO WA RAISI WA SERIKALI YA CHUO CHA SAUT, MARYGORETH GERVASE, ALISEMA KUWA WANAFUNZI WA KIKE WA CHUO HICHO WAMEKUWA WAKIKUTANA NA CHANGAMOTO ZA  KUPATA MIMBA ZISIZO TARAJIWA, NDOA ZA MUDA MFUPI WAWAPO SHULENI NA PIA USALAMA MDOGO KWA WASICHANA WANAO KUWA NJE YA CHUO.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA SAUTI.

No comments:

Powered by Blogger.