ZITTO KABWE AVULIWA RASMI UANACHAMA NDANI YA CHADEMA.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto
Kabwe amevuliwa rasmi uanachama ndani ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), baada
ya Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo kutupilia mbali kesi aliyokuwa ameifungua dhidi ya chadema akihoji uhalali wa uanachama wake ndani ya chama hicho.
Habari zinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na maendeleo Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama wa
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Akitangaza mapema leo hatua hiyo ya kumvua uanachama, Lissu
alisema kanuni na sharia za chama hicho ziko wazi na zinaelekeza kuwa endapo
mwanachama yeyote atakishtaki chama hicho mahakamani na iwapo atashindwa
atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye chama.
"Kwa
mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi
mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa
amejiondoa uanachama wake, kwa hiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio
mwanachama tena wa Chadema” Alisema Lissu.
Mbali na hayo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imeamuru CHADEMA
kulipwa gharama zote za kuendeshea case hiyo hiyo ikiwa na maana kwamba Zitto
anapaswa kulipa gharama zote za kesi hiyo na kwamba hakuna shauri lolote
Mahakamani kwa sasa.
Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha
Kamati Kuu kumjadili ambapo hoja yake ilikuwa kupinga kuitisha kamati kuu kabla
shauri lake halijasikilizwa na Baraza Kuu ambapo alitaka mahakama iagize kamati
kuu ya CHADEMA kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa
yake.
NA MHARIRI: BINAGI MEDIA GROUP KWA MSAADA WA MTANDAO.
No comments: