 |
Maandamano ya Akina Mama wakiingia katika uwanja wa Shule ya Sekondari Mogabiri Wilaya ya Tarime yalipofanyikia Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani katika ngazi ya Mkoa wa Mara juzi March 08, 2015. |
Na: George Binagi-GB Pazzo
Imeelezwa
kuwa Mkoa wa Mara unaongoza katika Vitendo mbalimbali vya Ukatili wa kijinsia
ikilinganisha na Mikoa Mingine hapa nchini, ambapo vitendo hivyo vimeelezwa
kufikia zaidi ya asilimia 66 katika Mkoa huo.
Hayo yalielezwa juzi na Yasin Ally ambae ni Mkurugenzi wa Shirika
la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana KIVULINI la Jijini Mwanza, katika Maadhimisho ya Siku
ya Wanawake duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Kijiji cha Mogabiri Wilaya ya
Tarime Mkoani Mara.
Yasini alibainisha kuwa Mkoa wa Mara unaongoza kwa tatizo la
vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ambapo Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia
vimefikia asilimia 66.4 ukifuatiwa na Mkoa wa Kagera wenye asilimia 46.4 huku
Mikoa ya Mwanza na Geita ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia 43.
Alizitaja baadhi ya aina za Ukatili wa Kijinsi zinazotendeka
katika Mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Ukatili wa Kingono, Kimwili, Kiuchumi
ambapo amefafanua kwamba Ukatili wa Kijinsia ni kitendo chochote kile
anachofanyiwa hadharani au kwa kificho mwanamke au mwanamke na hivyo
kumsababishia mauvimu ya kimwili, kihisia ama kisaikolojia ikiwa ni miongoni
mwa madhara mengine mengi yanayosababishwa na Ukatili wa Kijinsia.
Ili kutokomeza Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia, Ally alitaka
Ukatili wa kijinsia Kufichuliwa katika jamii kwa kiwango ambapo hatua za
kisheria zitachukuliwa ambapo ameliomba jeshi la Polisi sanjari na viongozi wa
Serikali za mitaa kuonyesha ushirikiano wao na wanajamii kwa lengo la
kuhakikisha kwamba Ukatili wa kijinsia unatokomezwa katika jamii.
Risala ya Wanawake katika Maadhimisho hayo ilieleza kuwa Mkoa wa
Mara unaongoza katika kila aina za Ukatili ambapo aina hizo ni pamoja na Vipigo
visivyo vya msingi kwa wanawake walio katika ndoa ambavyo vimepelea wanawake
wengi kusalia na ulemavu wa kudumu au vifo huku Risala hiyo ikibainisha kwamba
Ukatili mkubwa wa Kijinsia katika Mkoa wa Mara ni suala la Ukeketaji ambalo
limewaacha wasichana/ wanawake wengi katika madhara makubwa ikiwa ni pamoja na
Kupoteza damu nyingi, matatizo wakati wa kujifungua, maambukizi ya virusi vya
Ukimwi, ndoa za Utotoni pamoja na vifo wakati mwingine.
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mara Kaptaini Mstaafu Aseri
Msangi ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo ya Siku wa Wanawake
duniani katika Mkoa wa Mara, alieleza kusikitishwa kwake kutokana na vitendo
mbalimbali vya Ukatili vinavyoelezwa kutokea Mkoani Mara ikiwa ni pamoja na
Vitendo vya Ukeketaji ambavyo alieleza kusikitishwa kwake kutokana na kufanyika
hadharani.
Kutokana na hali hiyo alitoa wito Sheria Kuchukua Mkondo wake ili
kuzuia Ukatili wa Kijinsia ambapo alibainisha kuwa Bunge limetunga sheria
inayopinga Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni pamoja na Kuzuia Ukeketaji hivyo ni
vyema sheria hiyo ikatekelezwa ipasavyo ambapo aliwaonya wale wote wanaofanya
vitendo vya Ukeketaji tena hadharani kuwa sheria zitachukuliwa dhini yao huku
akiwahimiza Mahakimu kutoa adhamu kali kwa wote watakaofikishwa mahakamani
kutokana na kesi za Ukeketaji.
Aidha aliongeza kuwa Mwakani atatoa zawadi kwa
OCD (Mkuu wa Polisi Wilaya) atakaewafikisha wakeketaji (Mangariba) wengi
mahakamani.
Siku ya wanawake duniani ilianza kuadhimishwa duniani
mwaka 1911, wakati makundi ya wanawake nchini Marekani yalipokusanyika kupinga
udhalilishaji, ukandamizaji, uonevu na ubaguzi wa kijinsia hususan katika
sehemu za kazi. Nchini Tanzania Siku hii ilianza kuadhimishwa
mwaka 1997 katika ngazi ya Kitaifa na mwaka 2005 katika ngazi ya Kimikoa ambapo
baada ya hapo maadhimisho ya Kitaifa hufanyika kila baada ya Miaka Mitano na
kwa mwaka huu wa 2015 Siku ya Wanawake duniani Kitaifa ilifanyika Mkoani
Morogoro ikiwa na Kauli Mbiu isemayo “Uwezeshaji Wanawake, Tekeleza Wakati ni
Sasa”.
Kilele cha Siku ya Wanawake duniani hufanyika kila
Mwaka March 08 ambapo siku hii hutoa fursa kwa wanajamii, wafanyakazi wanawake,
taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali kufanya tathmini juu ya
masuala mbali mbali ya kimaendeleo kwa wanawake na hasa kuangalia matatizo
yanayowakabili na jinsi ya kuyatatua, kutafakari juu ya haki zao katika ajira
na jamii, kufanya tathmini juu ya mafanikio yao na kupanga mikakati mipya ya
kimaendeleo. Lengo kuu ni kuondoa vikwazo kwa wanawake katika nyanja za
kisiasa, kiuchumi na kijamii ili kujipatia maendeleo.
 |
Maandamano ya Akina Mama kutoka Halmashauri mbalimbali Mkoani Mara yakiingia katika uwanja wa Shule ya Sekondari Mogabiri Wilaya ya Tarime yalipofanyikia Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani katika ngazi ya Mkoa wa Mara juzi March 08, 2015. |
 |
Maandamano ya Akina Mama kutoka Halmashauri mbalimbali Mkoani Mara yakiingia katika uwanja wa Shule ya Sekondari Mogabiri Wilaya ya Tarime yalipofanyikia Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani katika ngazi ya Mkoa wa Mara juzi March 08, 2015. |
 |
Wawakilishi kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare Kilichopo Manispaa ya Musoma nao walikuwepo pia. |
 |
Wanafunzi ambao ni akina mama wa Kesho nao walikuwepo ili kujionea wenyewe utamu wa Shughuli ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani Wilayani Tarime Mkoani Mara. |
 |
Mkuu wa Mkoa wa Mara Kaptaini Mstaafu Aseri Msangi (katikati) ambae pia alikuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani Mkoani Mara. Kushoto ni Benedict Ole Kuyan ambae ni Katibu Tawala Mkoa wa Mara ambapo Kushoto ni Stanford Shayo ambae ni Katibu Tawala Halmashauri ya Mji wa Tarime |
 |
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mara. |
 |
Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Kenyamanyori iliyopo Wilaya ya Tarime Mkoani Mara wakisoma Shairi katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Kimkoa Mogabiri Wilaya ya Tarime Mkoani Mara. |
 |
Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Kenyamanyori iliyopo Wilaya ya Tarime Mkoani Mara wakikabidhi Shairi kwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Kimkoa Mogabiri Wilaya ya Tarime Mkoani Mara. |
 |
Wasomaji wa Risara ya akina Mama Mkoani Mara. |
 |
Mgeni Rasmi akipokea Risala ya akina Mama Mkoani Mara. |
 |
Wachezaji wa Ngoma ya Asili ya Irirandi kutoka kutoka Magatini Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara wakitoa burudani katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Mkoani Mara. |
 |
Wachezaji wa Ngoma ya Asili ya Irirandi kutoka kutoka Magatini Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara wakitoa burudani katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Mkoani Mara. |
 |
Baadhi ya Wanafunzi na Wanawake Mkoani Mara wakifuatilia matukio katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Kimkoa Mogabiri Tarime Mkoani Mara. |
 |
Baadhi ya Wanafunzi na Wanawake Mkoani Mara wakifuatilia matukio katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Kimkoa Mogabiri Tarime Mkoani Mara. |
 |
Baadhi ya Wawakilishi kutoka Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana Kivulini wakiwa katika banda la Shirika hilo. Kivulini walishiriki vyema katika kuhakikisha Maadhimisho hayo yanafanikiwa. |
 |
Mkuu wa Mkoa wa Mara Kaptaini
Mstaafu Aseri Msangi (alienyoosha Mkono jikoni) ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo ya Siku
wa Wanawake duniani katika Mkoa humo akikagua jiko la Ubunifu kutoka katika Kituo cha Maendeleo ya Kilimo Mogabiri Wilayani Tarime. |
 |
Jiko la Ubunifu kutoka katika Kituo cha Maendeleo ya Kilimo Mogabiri Wilayani Tarime. |
 |
Mkuu wa Mkoa wa Mara Kaptaini Mstaafu Aseri Msangi akikagua banda la Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Mara-Serengeti. Dayosisi hii kupitia katika kituo chake cha nyumba salama ya waliokimbia ukeketaji na ukatili wa kijinsia hutengeneza kazi mbalimbali za Mikono (Ujasiriamali) kama Mafuta na batiki. |
 |
Rhobi Samwel (Kulia) ambae ni Mrati wa Mpango wa Serengeti tunaweza bila Ukatili wa Kijinsia akionyesha Vipeperushi mbalimbali vinavyotolewa na Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Mara vyenye ujumbe juu ya Mpango wa Kupunguza Ukatili wa Kijinsia, Maambukizi Mapya ya Virusi vya Ukimwi na Ukeketaji vinavyoandaliwa na Kanisa hilo. |
 |
Noel Thobias ambae ni Mtengenezaji wa Kazi za Mikono (Ujasiriamali) akionyesha bidhaa mbalimbali zinazotengezwa na Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mara kupitia Kituo chake cha nyumba salama ya waliokimbia ukeketaji na ukatili wa kijinsia. |
 |
Mkuu wa Mkoa wa Mara Kaptaini
Mstaafu Aseri Msangi (Kulia) ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo ya Siku
wa Wanawake duniani katika Mkoa wa Mara akipokea maelezo kutoka kwa Asia Muya (Mwenye Kipaza Sauti) ambae ni Mratibu wa Mpango wa Kuzuia Ukatili wa Kijinsia kwa Watu walio katika Mahusiano (Mke na Mme) unaoratibiwa na Shirika la Kivulini. |
 |
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Kaptaini Mstaafu Aseri Msangi akifuatiwa na Stanford Shayo ambae ni Katibu Tawala Halmashauri ya Mji wa Tarime (Mwenye Kinasa sauti). |
 |
Mwenye kinasa sauti ni Benedict Ole Kuyan ambae ni Katibu Tawala Mkoa wa Mara ambapo aliekaa Kulia ni Kaptaini Mstaafu Aseri Msangi ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Mara. |
 |
Kaptaini Mstaafu Aseri Msangi ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Mara (Aliesimama) akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Kijiji cha Mogabiri Wilaya ya Tarime Mkoani Mara juzi Jumapili March 08.2015. |
No comments: