LIVE STREAM ADS

Header Ads

PICHA KUMI MUHIMU KATIKA ZIARA YA KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA WILAYANI MISUNGWI.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa waa Mwanza Miraji Mtaturu (Katikati walio mbele) juzi akiwa ameongozana na Diwani wa Kata ya Usagara Wilayani Misungwi Costantin Kilaga (Kushoto) pamoja na Katibu wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  UVCCM Mkoa wa Mwanza Issack Kalleiya katika ziara ya kukagua ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Sanjo iliyopo Kata ya Usagara Misungwi. Ili kufanikisha ujenzi huo, Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza kilichangia Mifuko thelathini ya Simenti (theluji) kwa ajili ya ujenzi wa maabara hizo.
Ziara ya Mtaturu ilianza Wilayani Misungwi Juzi Jumamosi March 28 na kuhitimishwa jana jumapili march 29 mwaka huu.
Na:George GB Pazzo
Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ukijionea ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Sanjo iliyopo Kata ya Usagara Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.
Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza ukikagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nyang'homango Kilichopo Usagara Wilayani Misungi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza akikagua mashine ya kufua umeme kwa ajili ya kusukumia maji kuelekea katika tank la Fela kwa ajili ya matumizi ya wananchi wa Kijiji cha Fela na pamoja na maeneo mengine katika Wilayani Misungwi.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza akikagua Tank la kuhifadhia maji katika Kijiji cha Fela Wilayani Misungwi kwa ajili ya matumizi ya wananchi kijijini hapo pamoja na maeneo mengine.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza akisalimiana na Wanakijiji pamoja na wanachama wa Chama hicho katika Kijiji cha Fela ulipo Mradi wa Maji Fela wakati alipofika Kijijini hapo kwa ajili ya Ukaguzi wa Mradi huo jana.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Simon Mayunga Mangelepa (Aliesimama) akitoa salamu zake katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Misungwi kilichofanyika hii leo jumapili katika Ukumbi wa CCM Wilayani Misungwi.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Aliesimama) akizungumza katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho katika Wilaya ya Misungwi ikiwa ni katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama katika miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani Misungwi.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Misungwi wakiwa katika Mkutano wao hii leo ambapo Katibu wa Chama hicho alikuwa akizungumza na wajumbe hao.
Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wakiwa katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Misungwi ambapo Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akizungumza na Halmashauri kuu ya CCM Wilayani Misungwi.
SOURCE: 99.4 RADIO METRO FM

No comments:

Powered by Blogger.