LIVE STREAM ADS

Header Ads

CCM YAZUIA KUFUNGWA KWA BARABARA YA AIRPORT-IGOMBE ILIYOPO ILEMELA MKOANI MWANZA.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akizungumza wiki iliyopita katika Eneo la barabara ya Airport-Igombe baada ya barabara hiyo kudaiwa kufungwa huku jeshi la wananchi likipewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa amri hiyo.
Na:George GB Pazzo
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza kimezuia Barabara ya Airpot hadi Igombe Wilayani Ilemela kufungwa, hadi pale barabara mbadala itakatengenezwa kwa lengo la kuondoa adha kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Zuio hilo lilitolewa na Miraji Mtaturu ambae ni Katibu wa chama hicho Mkoani Mwanza baada ya kupokea Malalamiko kuwa wananchi wanakosa huduma za kijamii kutokana na barabara hiyo kufungwa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Jengo la mizigo katika Uwanja wa ndege wa Mwanza.

Mtaturu alisema kuwa wakati ujenzi wa jengo hilo ukiendelea ni vyema wananchi wakaruhusiwa kuendelea kutumia barabara hiyo ya Airport-Igombe huku Serikali ikiendelea kutafuta barabara mbadala.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Manju Msambya aliahidi kushughulikia upatikanaji wa barabara mbadala kwa ajili ya kuwaondolea adha wananchi wa Igombe ambao awali walitakiwa kupita barabara ya Busweli yenye urefu wa Kilomita 25 hadi kufika Jijini Mwanza.


Nao baadhi ya wananchi walieleza kuwa Kufungwa kwa barabara hiyo ya Airport-Igombe ambayo ni kiunganishi kwa Kata nne za Wilaya ya Ilemela ambazo ni Kata ya Bugogwa, Shibula, Sangabuye pamoja na Kayenze kunaweza kuwaletea athari mbalimbali ambazo ni pamoja na athari za kiuchumi pamoja na ukosefu wa upatikanaji wa huduma za afya kwa haraka zaidi ambapo walisisitiza kwamba serikali inapaswa kuwajengea barabara mbadala itakayopita pembezoni mwa ziwa Victoria na kuungana na barabara ya inakwenda Malaika Hotel.
Kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwasikiliza wananchi katika eneo la Airport wiki iliyopita.
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Mh.Manju Msambya akiwa pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Katikati) walipotembelea barabara ya Airport-Igombe baada ya barabara hiyo kufungwa kutokana na kuanza kwa ujenzi wa jengo la mizingo na njia ya ndege za mizigo kukimbili katika Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Diwani wa Kata ya Bugogwa (CCM) ambae pia ni Naibu wa Meya wa Manispaa ya Ilemela Dede Swila Dede akionyesha namna barabara mbadala inavyopaswa kutengenezwa
Mkuu wa Wilaya ya llemela Manju Msambya akizungumza baada ya ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza kutembelea katika barabara ya Igombe-Airport ambayo ilikuwa imefungwa kutokana na ujenzi katika Uwanja wa ndege wa Mwanza na hivyo wananchi wa Igombe. Kayenze na maeneo mengine kutakiwa kutumia barabara ya Buswelu kuingia Jijini Mwanza kwa mwendo wa Kilomita 25 badala ya kilomita tano wanazoweza kutumia wakipita katika barabara hiyo ya Airpot-Igombe.
Wananchi wakiwa katika eneo la Airport wakimsikiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu baada ya kwenda kusikiliza malalamiko yao kutokana na kufungwa kwa barabara ya Airpot-Igombe kutokana na kuanza kwa ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Credit:Radio Metro

No comments:

Powered by Blogger.