LIVE STREAM ADS

Header Ads

HAKIKISHA UNAFIKA KATIKA BANDA LA SHIRIKA LA POSTA NCHINI, MWAUASA, KK SECURITY NA STARTIMES KATIKA MAONYESHO YA MAY MOSI MKOANI MWANZA.

Kesho Ijumaa 01.05.2015 Tanzania inatarajia kuungana na Mataifa mbalimbali duniani katika kusherehekea Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Maarufu kwa jina la MAY MOSI ambayo Kitaifa yanafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba Ilemela Mkoani Mwanza.
Katika kuelekea katika Maadhimisho hayo ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi, tayari Maonyesho mbalimbali yanaendelea katika Uwanja wa Furahisha Wilayani humo.
Kauli mbiu ya Maonyesho hayo nchini ni "Mfanyakazi Jiandikishe, Kura Yako Ina Thamani Kwa Maendeleo Yako".

Binagi Media Group hii leo imepata fursa ya kutembelea Mabanda mbalimbali katika Maonyesho hayo ya May Mosi yanayoendelea katika Uwanja wa Furahisha na Kuvutiwa na Mabanda Manne Bora Kabisa ambayo ni Banda la Shirika la Posta nchini, Banda la Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoani Mwanza MWAUASA, Banda la Kampuni ya Ulinzi KK Securit pamoja na Banda la Kampuni ya Visimbuzi ya StarTimes na kuridhishwa na Mabanda hayo hivyo kama hujafika katika maonyesho hayo hakikisha unaenda na kisha kufika katika mabanda hayo ili kujionea huduma na bidhaa kabambe zinazotolewa hapo.
Na:George GB Pazzo
Meneja wa Shirika la Posta nchini Julius Chifungo (Kushoto) akiwa pamoja na Tobietha Makafu (Kulia) ambae ni Afisa Mahusiano Mwandamizi wa Shirika hilo nchini Tanzania katika Maonyesho ya Mei Mosi yanayoendelea katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza.
Meneja wa Shirika la Posta nchini Julius Chifungo (Kulia) akiwa mahojiano na Mwandishi/ Mtangazaji wa Metro Fm Alphonce Tonny Kapela Dr.Tonny (Kushoto) kuhusiana na Maonyesho hayo.
Kutoka Kushoto ni Mwandishi/ Mtangazaji wa Metro Fm Alphonce Tonny Kapela Dr.Tonny akifuatiwa na Meneja wa Shirika la Posta nchini Julius Chifungo, anaefuatia ni Katumba Madua a.k.a Mc Karumba Mtangazaji Radio Metro na wa mwisho ni Tobietha Makafu ambae ni Afisa Mahusiano Mwandamizi wa Shirika la Posta nchini.
Watumishi wa Shirika la Posta nchini.
Baadhi ya wananchi waliofika katika Maonyesho ya Mei Mosi wakipata maelekezo kutoka katika Banda la Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoani Mwanza MWAUASA.
Alphonce Tonny Kapela a.k.a Dr.Tonny (Kushoto) kutoka Radio Metro akifanya Mahojiano na Eng.Gombela Henry Nswila (Kulia) ambae ni Mkuu wa Kanda ya Makongoro kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoani Mwanza MWAUASA.
Waliosimama ni Alphonce Tonny Kapela a.k.a Dr.Tonny (Kushoto) kutoka Radio Metro akifanya Mahojiano na Eng.Gombela Henry Nswila (Kulia) ambae ni Mkuu wa Kanda ya Makongoro kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoani Mwanza MWAUASA.
Eng.Wilberg Bujiku kutoka MWAUASA kitengo cha MajiTaka (kulia) akiwa pamoja na Eng.Juma Pazi (kushoto) kutoka MWAUASA pia kitengo cha Mitambo na Umeme.
Banda la Mamlaka ya Maji Safi na MajiTaka MWAUASA Mkoani Mwanza ambapo Kulia ni Mc Katumba kutoka Radio Metro akisaini Kitabu cha Wageni na Kushoto ni baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo.
Katika picha anaonekana Albert Isack ambae ni Afisa Mauzo kutoka Kampuni ya Ulinzi ya KK Security Kanda ya Ziwa akitoa ufafanuzi wa huduma za Kampuni hiyo katika Maonyesho ya Mei Mosi yanayoendelea katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza. Kampuni hii inatoa huduma ya Ulinzi wa aina mbili ambao ni Ulinzi wa Maaskari wanaotumia Virungu, Bunduki na Mbwa pamoja na Ulinzi wa Mitambo ya Kisasa kabisa.
Ukifika katika Maonyesho haya ya Mei Mosi,tembelea katika banda la StarTimes ambapo utaweza kuhudumi vyema kabisa na hivyo kuelewa mambo mengi ambayo huyajui kuhusiana na Mfumo wa Urushaji wa Matangazo ya Tv kwa mfumo wa Kisasa ikiwa ni pamoja na Kujipatia Ving'amuzi vya StarTimes ili nawe upate kufurahia Ulimwengu wa Dijitali nchini Tanzania.
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTIONS

No comments:

Powered by Blogger.