KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA ATOA AGIZO KWA MANISPAA YA ILEMELA.
Na:George GB Pazzo
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza
imetakiwa kurekebisha daraja la Msuka lililopo Kilimahewa, linaunganisha
barabara ya Isanga Kiloleni ili kuondoa adha wanayoipata watumiaji wa barabara
hiyo wakati wa Mvua.
Katibu wa Chama cha
Mapinduzi Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara
ya kutembelea daraja hilo, wakati wa ziara yake ya kukagua Miradi ya Maendeleo
Wilayani Ilemela.
Wakati wa mvua
daraja hilo huwa halipitiki kutokana na maji kujaa na kupita juu yake, na hivyo
kuzagaa ovyo hadi katika nyumba na makazi ya wananchi.
Katika hatua
nyingine, Mtaturu alitoa muda wa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilemela iwe imejenga daraja la Ujiji linalopitisha Maji ya Mto Msuka liwe limejengwa
baada ya kubomolewa na Maji ya Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Mwanza na
hivyo kuhatarisha maisha ya watumiaji wake hususani wanafunzi wa shule za
msingi.
Kwa Upande wa
Daraja la Msuka, Mhandisi wa Barabara kutoka Manispaa ya ilemela Mikidadi Adam alisema
kuwa Manispaa hiyo iko katika hatua za mwisho za kumpata Mkandarasi kwa ajili
ya kurekebisha changamoto za Miundombinu zilizopo katika Manispaa hiyo, hivyo
ndani ya miezi mitatu miundombinu yote katika Manispaa hiyo likiwemo daraja la
Msuka itakuweza kurekebishwa.
No comments: