LIVE STREAM ADS

Header Ads

KWA HALI HIII, TFF INASTAHILI KUBEBESHWA ZIGO LA LAWAMA.

Zoezi limeishia hapa katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Na:Genya Richard-Mwanza
Shirikisho la soka Tanzania TFF limekwama kutoa nyasi bandia kutoka katika Bandari ya Dar es laam ikiwa ni nyasi za msaada kutokana Shirikisho la Soka la Kimataifa FIFA.

TFF iliomba msaada huo wa nyasi kwa ajili kuziweka kwenye viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza na Kaitaba Mjini Bukoba ambapo hali imekuwa tete na hivyo TFF kuomba msaada wa kusamehewa kodi na Serikali kama ambavyo ilifanya kwa nyasi za Uwanja wa Gombani, Karume na Uhuru.

Rais wa Shirikisho hilo la Soka nchini TFF Jamal Malinzi alisema kuwa TFF imekuwa ikikumbana na vikwazo vingi na hivyo kushindwa kutoa bandarini vifaa vya michezo vinavyowasili nchini kwa msaada kutokana na kodi huku pia akiongeza kuwa TFF iamemuomba Waziri wa Habari na Michezo Dk. Fenella Mkangara kuisaidia kusamehewa Kodi ya Vifaa vinavyowasili nchini kwa msaada.

Kauli yangu kama Mwandishi na Mtangazaji wa Michezo ni kwamba “Kwa hali hiyo inakuwa ni aibu kubwa kwa TFF kwa kuwa imeomba msaada imepewa lakini kuutoa Bandarini imeshindwa kwa kisingizio cha kodi, vipi kama mngeambiwa kuwa nyasi hizo mnapaswa kuzinunua wenyewe, mngeweza?

Wizara ya Michezo na Mtamaduni ondoeni aibu hii pale bandarin kwani vijana wetu wanataka wacheze mpira kwenye viwanja vizuri na vyenye kuvutia hivyo msiwategemee TFF katika hili kwa kuwa kazi imewashinda na hivyo kukubali kubebeshwa zigo la lawama”.

Hata hivyo haijabainika wazi ni kiasi gani cha Fedha kinachohitajika kwa ajili ya kulipia kodi ya Nyasi hizo bandia ambazo zimekwama Bandarini, japo ni vigumu kwa wanamichezo kuamini kwamba TFF imeshindwa kujichanga na kupata fedha hizo kwa ajili ya kuzitoa Bandarini ili Uwekaji wa Nyasi katika Viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza na Kaitaba Mkoani Kagera uweze kukamilika kwa wakati.
                                        BONYEZA HAPA KUJIONEA UJENZI ULIVYOANZA KWA KASI

No comments:

Powered by Blogger.