LIVE STREAM ADS

Header Ads

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA MKOANI MWANZA ATAKIWA KUTAFUTA KAZI NYINGINE.

Wananchi na Makada wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza wakiwa katika Mkutano wa hadhara juzi uliofanyika katika Uwanja wa Magomeni Kata ya Kirumba Wilayani Ilemela ambapo Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akihutubia ikiwa ni katika kuhitimisha ziara yake ya kutembela Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza aliyoianza March 22 mwaka huu katika Wilaya ya Ukerewe. Kabla ya Mkutano huo pia Mtaturu alipata fursa ya Kukagua Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Ilemela ikiwa ni katika Kujionea utekelezaji wa Ilani cha Chama cha Mapinduzi
Na:George GB Pazzo
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza Highness Kiwia (Chadema) ametakiwa kutafuta kazi nyingine ya kufanya na si siasa kwa kuwa kazi hiyo imemshinda.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alipokuwa aliwahutubia wananchi na Makada wa Chama hicho katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Magomeni Kirumba jimboni humo.

Mtaturu alisema kuwa mbunge huyo ameshindwa kutekeleza kazi aliyoagizwa na wananchi wa Ilemela, badala yake amegeuka kutekeleza maagizo anayopewa na Mwenyekiti wa Chama chake Taifa Freema Mbowe huku akiwasahau wananchi waliomchagua.

"Wananchi walimchagua ili awatumikie ikiwa ni pamoja na kwenda kuwasemea bungeni...lakini Mbowe akimzuia kuingia bungeni nae kweli haingii, kwa maana hiyo wanailemela eleweni kuwa hamna mtu wa kuwasemea bungeni". Alisema Mtaturu huku akiongeza kuwa mbunge huyo anapaswa kutafuta kazi nyingine ya kufanya maana ubunge umemshinda na wananchi pia wamemchoka.

Mtaturu aliongeza kuwa mbunge huyo ameshindwa kusimamia vyema majukumu yake ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Maabara, ukarabati pamoja na ujenzi wa Miundominu ya barabara, majukumu ambayo kwa sasa yanatekelezwa na Chama cha Mapinduzi.

Aidha aliwasihi wananchi mwaka huu kuhakikisha kuwa wanakichagua Chama cha Mapinduzi CCM huku akibainisha kuwa katika uchaguzi Mkuu uliopita wa mwaka 2010 Chama hicho kiligawa jimbo kutokana na migogoro ya ndani ya chama jambo ambalo alisema kuwa halitajirudia tena mwaka huu.

Baadhi ya Wananchi waliozungumza na Binagi Media Group walieleza kuwa uwezekano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ilemela kurejea Madarakani Jimboni humo ni mdogo ukilinganisha na vyama vingine ikiwemo CCM, kutokana na ubovu wa miundombinu shughuli nyingi za kimaendeleo kushindwa kutekelezeka katika jimbo hilo baada ya Chadema kuingia madarakani.

Binagi Media Group ilipomtafuta Kiwia ambae kwa muda mrefu hajaonekana jimboni kwake ili kuzungumzia kauli ya Mtaturu, Simu yake ya Mkononi haikuweza kupatikana baada ya namba yake ya simu inayoishia 070 anayoitumia kutopatika hewani kwa muda mrefu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (katikati) akisalimiana na Wananchi pamoja na Makada wa CCM Mkoani Mwanza baada ya kuwasili katika Uwanja wa Magomeni Kirumba Wilayani Ilemela ambapo alikuwa na Mkutano wa hadhara.
Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela Nelson Mesha akifuatiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu na wa tatu kutoka kushoto akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Manju Msambya.
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza pamoja na Viongozi wa Serikali Wilayani Ilemela.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata (Mwenye Vinasa sauti) akitoa salamu zake katika Mkutano wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza uliofanyika juzi Magomeni Kirumba.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa akitoa salamu zake katika Mkutano wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza uliofanyika juzi Magomeni Kirumba.
Mwajuma Mboha (Kushoto) akitoa salamu zake katika Mkutano wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza uliofanyika juzi Magomeni Kirumba. Kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa 
Batazari Bosco ambae ni akitoa salamu zake kwa niaba ya wanafunzi Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka Vyuo mbalimbali vilivyopo Mkoani Mwanza ikiwemo SAUT pamoja na CBE. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela Nelson Mesha.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwahutubia wananchi wa Ilemela na Maeneo jirani katika Mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika Uwanja wa Magimeni Kirumba Wilayani humo.
Wanchi na Makada wa CCM Wakimsikiliza kwa Makini Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akihutubia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika Uwanja wa Magomeni Kirumba Wilayani Ilemela.
Credit:Binagi Media Group & Radio Metro Fm

No comments:

Powered by Blogger.