LIVE STREAM ADS

Header Ads

HOSIPITALI YA WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA YAPONGEZWA.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwasili jana Mantare Jimbo la Sumve Wilayani Kwimba kwa ajili ya Mkutano wa Hadhara.
 Na:George GB Pazzo
Hospitali ya Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza imepongezwa kwa namna ambavyo imeboresha huduma zake za Afya kwa Wananchi, hususani huduma za wazee kupitia dirisha la wazee pamoja na huduma ya Mama na Mtoto.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alitoa kauli hiyo jana alipotembelea Hospital hiyo, ikiwa ni katika kuhitimisha ziara yake ya Siku mbili aliyoianza juzi jumatatu Wilayani humo.

Alisema kuwa pamoja na kwamba wahudumu wa afya katika Hospitali hiyo ni wachache lakini ni vyema ikahakikisha kuwa inaweka utaratibu mzuri ili kuhakikisha kuwa huduma za Afya zinapatikana kwa wananchi hospitalini hapo muda wote.

Mtaturu aliipongeza Hospitali hiyo kwa namna ambavyo imeboresha huduma ya Mama na Mtoto pamoja na Wazee kupitia huduma ya dirisha la Wazee, ambapo amesema kuwa Wilaya ya Kwimba ni miongoni mwa Wilaya chache zilizofanikiwa kuboresha huduma hizo hivyo amezitaka hospitali nyingine kuiga mfano huo.

Katika hatua nyingine Mtaturu aliushauri uongozi wa hospitali hiyo kumtafuta Mkandarasi kwa ajili ya Kushughulikia huduma ya Usafi hususani usafi wa Vyoo hospitalini hapo, badala ya kuwategemea wauguzi wa hospitali hiyo hali ambayo inaongeza uzito wa majukumu na hivyo kufanya hospitali hiyo hususani vyoo kuwa katika hali mbaya ya uchafu kama alivyojionea katika ziara yake hospitalini hapo.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr.Paul Swakala alibainisha kuwa hospitali hiyo imekuwa na dhamira ya dhati katika kuhakikisha kuwa inaboresha huduma za afya, ambapo aliwaomba wadau wa Afya kujitokeza kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa Vifaa afya kwa ajili ya wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo ujenzi wake ulikamilika tangu mwaka jana lakini haijaanza kufanya kazi kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo.

Kuhusu huduma za afya kwa wazee kupitia dirisha la wazee, Dr.Swakala alisema kuwa Wazee wengi wanaotibiwa hospitalini hapo  wamekuwa wakitiwa bure kupitia kibali cha msamaha wanachoandikiwa wanapofika hospitalini wakiwa na barua ya mtendaji ambapo amebainisha kuwa Hospitali hiyo imeandaa utaratibu wa kuanza kuwasajili wazee Wilayani Kwimba kwa ajili ya kuwapatia kadi za matibabu kupitia dirisha la wazee.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wakipata matibabu hospitalini hapo walielezea kupata huduma nzuri za matibabu hospitalini hapo, ambapo waliomba huduma hizo kuendelea kuboreshwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba madaktari wanakuwepo hospitalini hapo muda wote.

Hatimae ziara hiyo pia ilielekea katika Hospitali teule ya Sumve Wilayani Kwimba ambayo ni ya Mission na kuupongeza pia Uongozi wa Hospitali hiyo kwa namna ambavyo umekubali kushirikiana na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma za Afya kwa Wananchi.

Akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Uchaguzi la Kwimba katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Stand ya zamani ya Ngudu siku ya Juzi Jumatau pamoja na Mkutano kama huo uliofanyika jana jumammne katika Kijiji cha Mantare Jimbo la Uchaguzi la Sumve, Katibu huyo wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alisema kuwa pamoja na mambo mengine ziara yake Wilayani Kwimba imelenga kuwakumbusha wananchi wakati utakapofika wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kupata fursa ya kushiriki katika zoezi la kupiga kura katika Kura ya maoni ya Katiba mpya pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Leo Mtaturu anatarajia kuanza ziara yake ya Siku mbili Wilayani Magu ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza ambazo pamoja na mambo mengine zimelenga kujitambulisha kwake kwa wananchi na wanaccm baada ya kuwasili Mkoani Mwanza akitokea Mkoani Iringa, pamoja na kutembelea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo Wilaya hizo kwa ajili ya kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2010/15.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Katikati) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Pili Moshi Bayo (Kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kwimba Petro Muyanga (Kushoto) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana Mantare Jimboni Sumve.
Katibu wa CCM Mkoani Mwanza akiwahutubia wananchi Jimboni Sumve jana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza (Kulia) akimpongeza Esther Sodoka (Kushoto) ambae ni Diwani wa Viti Maalumu (CCM) Tarafa ya Sumve kutokana na juhudi zake katika maendeleo ya Tarafa hiyo. Hii ilikuwa jana katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Jimboni Sumve.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akikagua mradi wa Maji katika Mji wa Ngudu Wilayani Kwimba.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akimtishwa mwanamama wakati alipotembelea Mradi wa Maji katika Mji wa Ngudu Kwimba siku ya jana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akiwa pamoja na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Pili Moshi Bayo (Mwenye Mkoba) wakipokea maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba Dr.Paul Swakala (Kulia).
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Katikati) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Pili Moshi Bayo (Kulia) wakimjulia hali wagonjwa katika Wodi ya akina mama katika Hospitali ya Kwimba. 
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (katikati) baada ya kufika katika Wodi ya akinamama alikuta kuna baadhi ya akinamama waliojifungua usiku wa kuamkia jana na hivyo akaomba mmoja wa watoto hao aitwe jina lake. Na hapa akimtazama Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Pili Moshi Bayo (kushoto) baada ya kumzawadia mtoto aliezaliwa Shilingi Elfu ili akubali kuitwa jina la lake.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwa pamoja na Msafara wake katika jengo jipya la Wagonjwa mahututi (ICU) lililopo katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba. Jengo hili lilikamilika tangu mwaka jana lakini halijaanza kutumika kutokana na kukosekana kwa vifaa ambapo Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Paul Swakala aliomba wadau kujitokeza kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa vifaa hivyo.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ikiwa katika Shule ya Sekondari Mwagi Iliyopo Sumve Wilayani Kwimba.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akikagua Ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Mwagi iliyopo Sumve Wilayani Kwimba ambapo kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Mtaturu aliahidi kutoa shilingi Milioni Moja kwa ajili ya Kusaidia kukamilisha Ujenzi wa Maabara katika shule hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Aliembeba Mtoto) akiwa pamoja na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mkoa wa Mwanza Simon Mayunga Mangelepa wakimzawadia Mtoto (Aliebebwa) baada ya kucheza vyema na kwa hisia kali wimbo wa Marehemu Komba uitwao CCM ni Ile ile.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akimzawadia Mtoto baada ya kucheza vyema wimbo wa Marehemu Komba alitembelea Jimbo la Sumve Wilayani Kwimba. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Kwimba Pili Moshi Bayo akifurahia ucheshi wa mtoto huyo.
SOURCE:99.4 RADIO METRO FM

No comments:

Powered by Blogger.