LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZAZI WA WANAFUNZI AMBAO BADO HAWAJARIPOTI SHULENI WILAYANI MAGU KUTIWA NGUVUNI.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akizungumza jana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitumba iliyopo Kisesa Wilani Magu alipotembelea Shule hiyi katika ziara yake ya Siku mbili iliyoanza jana.
 Na:George GB Binagi
Wazazi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza ambao hadi sasa hawajaripoti Shuleni kwa ajili ya kuanza Masomo yao, wametakiwa kukamatwa ili kueleza wanafunzi hao walipo.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alitoa kauli hiyo jana, alipotembelea Shule ya Sekondari Kitumba iliyopo Kata ya Kisesa Wilayani Magu wakati akiwa katika ziara yake ya Siku mbili Wilayani humo.

Mtaturu alisema ni lazima wazazi wa wanafunzi ambao ambao hadi sasa hawajaripoti Shuleni wakamatwe ili keleza wanafunzi ambao hawajaripoti Shuleni, kwa sababu baadhi ya wazazi wamewaozesha watoto wao na hivyo kuwanyima fursa ya kupata elimu.
Katika shule hiyo ya Katumba, takribani wanafunzi 10 wa kike ilielezwa kuwa hawajaripoti shuleni kwa ajili ya kuanza masomo yao, ambapo Mtaturu alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Magu Karen Yunus kwa kushirikiana na uongozi wa Shule hiyo ili kuhakikisha kuwa wazazi wa wanafunzi hao wanakamatwa kwa ajili ya kueleza wanafunzi hao walipo.

Katika hatua nyingine Mtatuturu alisema kuwa katika Sekta ya Elimu, Ilani ya Chama cha Mapinduzi imetekelezwa vizuri hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa ongezeko la ujenzi wa Shule za Sekondari ambapo Wilaya ya Magu peke yake ina Shule za Sekondari 26 ikilinganishwa na Shule nne za Sekondari zilizokuwepo katika Mkoa mzima wakati nchi iapata uhuru.

Akiwa katika Shule hiyo (Shule ya Sekondari Kitumba), Mtaturu aliahidi kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza  kutoa Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya Kusaidia kukamilisha ujenzi wa Maabara katika shule hiyo pamoja na kuweka Umeme wa Mionzi ya Jua (Sola) katika jengo la Utawala wakati mikakati ya kufikisha Umeme wa Tanesco shuleni hapo ikifanyika.

Ziara hiyo iliambatana na zoezi la Upandaji wa Miti katika Shule ya Msingi na Sekondari Kitumba ikiwa ni katika kusherehekea Siku ya Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi nchini, ambapo Kiwilaya katika Wilaya ya Magu Siku hiyo iliadhimishwa katika Uwanja wa Red Cross Kisesa.

Katika Sherehe hiyo ya Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Magu, Mtaturu aliwakabidhi wanachama wapya 23 ambao ni wa kike kadi za chama hicho huku akimkabidhi Antony Charles ambae alikuwa ni kiongozi na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema tangu mwaka 200 baada ya kurudisha kadi ya chama hicho.

Awali Mtaturu pia alifanya ziara katika Kituo cha Afya Kisesa Wilayani Magu ambapo aliipongeza Serikali kwa namna ilivyoboresha kituo hicho, huku akiagiza chombo cha  kuchomea taka katika kituo hicho kitengenezwe haraka iwezekanavyo ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza.

Akizungumza katika Kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Magu, Mtaturu alisema kuwa dhumuni la Chama hicho ni kushika dola kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania ambapo kuhusu tatizo la maji lililopo katika Wilaya hiyo alisema kuwa ni lazima lishughulikiwe ikiwa ni pamoja na kukamilisha Mradi wa Maji ambao ulianza kuahidiwa tangu uongozi wa Rais wa awamu ya Tatu Benjamini Mkapa hadi katika Uongozi wa awamu hii ya nne wa Jakaya Mrisho Kikwete.

Akifungua Shina la Wakeleketwa wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi UVCCM Stand ya Kisesa lenye wanachama zaidi ya 200, Mtaturu aliwataka vijana kuachana na ushabiki wa kisiasa ikiwa ni pamoja na kuepukana na baadhi wanasiasa wanaowatumia kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe.

Aliwaahidi Vijana hao kuimarisha Umoja wao ikiwa ni pamoja na kusajili kikundi chao ili kitambulike rasmi, lengo likiwa ni kuwasaidia fedha Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kuimarisha Miradi yao ya Ufugaji wa Kuku pamoja na uoshaji wa Magari (Car Wash) huku akiongeza kuwa baada ya Umoja huo kuwa imara atawaunganisha na taasisi za Mikopo ili waweze kukopa pikipiki zenye riba nafuu.

Leo Mtatu yuko Wilayani Magu akihitimisha ziara kama hiyo ambayo aliianza jana ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajia kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi tangu mwaka 2010/15 pamoja na kuwahutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Magu kuanzia majira ya saa nane mchane.
Mwalimu Murwani Segesa ambae ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kitumba Ilipo Kisesa Wilayani Magu akitoa taarifa fupi kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Hayuko pichani) alipotembelea shule hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitumba wakimsikiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Hayuko pichani) alipotembelea shule hiyo jana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akishiriki jana zoezi la upandaji miti katika shule uya Sekondari Kitumba Iliyopo Kisema Magu
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akishiriki jana zoezi la upandaji miti katika shule uya Sekondari Kitumba Iliyopo Kisema Magu.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mayunga Mangelepa akishiriki jana zoezi la upandaji Miti katika Shule ya Sekondari Kitumba Magu.
Mkuu wa Wilaya ya Magu Karen Yunus akishiriki zoezi la Upandaji Miti katika shule ya Sekondari Kitumba iliyopo kisesa Magu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akizungumza jana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitumba iliyopo Kisesa Magu baada ya kushiriki zoezi la upandaji miti katika shule hiyo ambapo zaidi ya Miche 400 ya miti ya aina mbalimbali ilipandwa.
Dr.Mecktrida Luhanga ambae ni Mganga Mkuu katika Kituo cha Afya Kisesa Wilayani Magu akisoma taarifa ya Kituo hicho wakati Katibu wa CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu alipotembelea kituo hicho.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akikagua jengo la UTRA SOUND NA EXRAY. Jengo hili halijakamilika hali ambayo ilipelekea mfadhiri aliesaidia vifaa vya Utra Sound pamoja na Exray kutishia kucghukua vifaa hivyo na kuvipeleka  Hospitali nyingine Mkoani Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwajulia hali wagonjwa katika kituo cha Afya Kisesa siku ya jana alipofanya ziara kituoni hapo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwa amembeba mmoja wa watoto mapacha waliozaliwa jana majira ya saa tano asubuhi alipotembelea katika Kituo cha Afya Kisesa Wilayani Magu. Mama wa Mtoto huyu alikubali mwanae kuitwa jina la Mtaturu.
Antony Liaya ambae ni Mwenyekiti wa Shina la Wakeleketwa wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi UVCCM Stand ya Kisesa lenye wanachama zaidi ya 200, jana akisoma Risala ya Shina hilo kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu jana akizindua Shina la Wakeleketwa wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi UVCCM Stand ya Kisesa lenye wanachama zaidi ya 200.
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza jana wakiwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Magu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akizungumza jana katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Magu.
Wajumbe mbalimbali wakiwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Magu.
Watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu wakiwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilayani humo.

No comments:

Powered by Blogger.