LIVE STREAM ADS

Header Ads

KIONGOZI MUHIMU WA CHADEMA ATIMKIA CCM. WENGINE 23 WAPYA NAO WAKABIDHIWA KADI ZA CCM.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akimkabidhi Kadi ya CCM aliekuwa Kada na kiongozi wa Chadema Katika Mikoa ya Mwanza na Katavi.
Na:George GB Pazzo
Aliekuwa Kada na Kiongozi katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema katika Mikoa wa Mwanza na Katavi Antony Charles Nongo, amekihama chama hicho na Kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.
Nongo alikuwa ni mwanachama wa Chadema tangu mwaka Elfu mbili na alifanikiwa kushika nyazifa mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho ambazo ni pamoja na Katibu Kata ya Buswelu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kabla ya kuhamia Mpanda Mkoani Katavi.

Akiwa Mpanda alikuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo pia alikuwa ni Meneja wa Kampeni za Uchaguzi mdogo uliopita wa Serikali za Mitaa kupitia Ukawa, huku pia akichaguliwa kuwa Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Mchangani Wilayani Mpanda baada ya Chama chake kutwaa Uongozi wa Kijiji hicho.

Akizungumza wiki iliyopita wakati akipokea kadi ya CCM, Nongo alisema kuwa amefikia maamuzi ya kutimka kutoka Chadema baada ya kubaini kwamba chama hicho kipo kwa ajili ya Maslahi, jambo ambalo linapelekea baadhi ya makada wake kutumika kwa ajili ya Maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa Chama hicho.

Alisema kuwa pamoja na kuitumikia Chadema Usiku na Mchana lakini amejikuta akikosa msaada kutoka ndani ya Chama hicho kutokana na kuuguliwa kwa muda mrefu na Mkewe ambapo ameongeza kuwa licha ya kuwa na mawasiliano mazuri na Viongozi wa Chama hicho bado hakupata ushirikiano wowote uliolenga kumsaidia mkewe kupata matibabu.

Nongo alikabidhiwa kadi ya Chama cha Mapinduzi wiki iliyopita katika Uwanja wa Msalaba Mwekundu Kisesa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu aliekuwa na ziara ya siku mbili Wilayani Magu ambapo pia Wanachama wapya 23 wa Kike waliweza kujiunga na CCM Wilayani Magu  na kukabidhiwa kadi za uanachama.
MSIKILIZE HAPA CHINI ANTONY CHARLES

Antony Charles Nongo akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi wa CCM wiki iliyopita katika Uwanja wa Msaba Mwekundu Kisesa Magu.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akimkabidhi kadi mmojwa wa mabinti waliojiunga na chama hicho wiki iliyopita ambapo mabinti 23 walijiunga na CCM na Kukabidhiwa kadi katika Uwanja wa Msalaba Mwekundu Kisesa Wilayani Magu.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akimkabidhi kadi mmojwa wa mabinti waliojiunga na chama hicho wiki iliyopita ambapo mabinti 23 walijiunga na CCM na Kukabidhiwa kadi katika Uwanja wa Msalaba Mwekundu Kisesa Wilayani Magu.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akimkabidhi kadi mmojwa wa mabinti waliojiunga na chama hicho wiki iliyopita ambapo mabinti 23 walijiunga na CCM na Kukabidhiwa kadi katika Uwanja wa Msalaba Mwekundu Kisesa Wilayani Magu.
Wasichana waliokabidhiwa kadi za Chama cha Mapinduzi CCM wakila kiapo cha uaminifu kwa ajili ya kukitumikia chama hicho.
Rebeca Nkulula akisoma Risala ya Wasichana ya wasichana 23 waliojiunga na CCM wiki iliyopita Wilayani Magu. Haijawahi kutokea Risala kusomwa mstari kwa Mstari, neno kwa neno lakini siku hiyo iliwezekana bada ya binti huyu kusoma Risala nzima aliyokuwa ameikariri kichwani.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwasili katika Uwanja wa Msalaba mwekundu Kisesa Wilayani Magu ambapo pia Maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya ya wazazi wa CCM Kiwilaya yalifanyikia.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akihutubia katika Uwanja wa Msalaba Mwekundu Kisesa Wilayani Magu yalipofanyikia Maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya ya wazazi wa CCM Kiwilaya yalifanyikia.
Wananchi wakimsikiliza Katibu wa CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu (Hayuko pichani) katika Viwanja Msalaba Mwekundu Kisesa Wilayani Magu.
Wachezaji wa Mpira wa Pete kutoka Timu Kisesa wakijiandaa kwa ajili ya Mchezo wao wa Kirafiki na Timu ya Bujora.
Wachezaji wa Mpira wa Pete kutoka Timu Bujora wakijiandaa kwa ajili ya Mchezo wao wa Kirafiki na Timu ya Kisesa.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatuturu akisalimiana akisalimiana na Timu ya Watoto Kisesa.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akiwa tayari kuzindua mchezo wa Mpira wa pete baina ya Timu ya Kisesa na Bujora.
Hapa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatuturu alikosa gori
Hapa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatuturu akielekeza mpira langoni.
Hapa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatuturu akizamisha mpira.
Miraji Mtaturu akionyesha uwezo wake.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akijiandaa kupiga Mpira kama ishara ya uzinduzi wa mechi kati ya Kisesa na Bujora iliyochezwa katika Uwanja wa Msalaba Mwekundu Kisesa Wilayani Magu.
Goooooooooooo.................Hatimae Miraji Mtaturu akazamisha Mpira wavuni.
SOURCE:99.4 RADIO METRO FM

No comments:

Powered by Blogger.