LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKATABA WA NGASSA KWISHA SASA ANAPIGA DEIWAKA YANGA.

Na:Genya Richard
Imebainika kwamba Kuanzia jana April 20 Mrisho Ngassasi ambae ni mchezaji wa Timu ya Soka ya Yanga Sport Club, anapiga deiwaka (anaitumikia Yanga bila Mkataba) katika Klabu hiyo kufuatia kumalizika kwa mkataba wake.

Hata hivyo kwa mjibu wa kanuni za soka Ngassa ataendelea kuichezea timu hiyo hadi kumalizika msimu huu kwa kuwa amesajiliwa kuichezea Yanga katika mashindano yote ya ndani na nje ya nchi.

Binagi Media Group kitengo cha Michezo jana April 20 kiliarifiwa kuwa Ngassa alimaliza mkataba  wake wa miaka miwili na Yanga na hajasini mkataba mpya.

“Kwa sasa sitaki kuzungumzaia masuala ya mkataba, nataka nimalize msimu kabisa ndiyo nianze mjadala wa mkataba mpya. Mimi ni mchezaji niliyesajiliwa Yanga msimu huu hivyo baada ya msimu kuisha ndipo mambo mengine yatafuata”. Alisema Ngassa wakati akizungumza na Binagi Media Group.

Kuhusu uvumi kuwavamesaini timu ya Free State ya Afrika kusaini, Ngassa alisema “Nipo kwenye mazungumzo na timu  tatu ikiwemo hiyo ya Free State na nyingine ya Qatar na pia nimeletewa ujumbe kwamba As Vita ya Congo na Etoile ya Tunisia nao wananifuatilia. Lakini mimi sina papara kwani nasubiri nimalize msimu wangu kwanza” Alisema Ngassa huku akisisitiza kuwa atakuwa tayari kuzungumzia masuala ya mkataba mpya baada kumalizika kwa msimu wa Soka wa Mwaka 2014/15.
                              BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTION

No comments:

Powered by Blogger.