LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTATURU ASEMA WASICHANA NA WANAWAKE AMBAO HAWAKUANDALIWA VYEMA NI TATIZO KWA TAIFA.

Wasichana kutoka Vyuoni, Shule za Sekondari na Majumbani kutoka Maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Sengerema wakiwa katika Kongamano la Wasichana lililofanyika Ijumaa wiki iliyopita, Kongamano hilo liliandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi UWT.
 Na:George GB Pazzo
Imeelezwa kuwa Wasichana pamoja na Wanawake ambao hawakuandaliwa vyema kwa kufundishwa misingi bora wa maadili katika Maisha yao, wamekuwa ni chanzo kikubwa cha Machafuko na migogoro katika Familia mbalimbali hapa nchini na Taifa kwa Ujumla.

Hayo yalielezwa ijumaa iliyopita na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu, wakati akifungua Kongamano la Wasichana Wilayani Sengerema kwa niaba ya Amina Makilagi ambae ni Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama hicho UWT.

Mtaturu alisema kuwa baadhi ya familia hapa nchini zimeingia katika migogoro mikubwa na hatimae kusambaratika kutokana na wanawake wanaoolewa katika familia hizo kutoandaliwa  vizuri katika misingi na maadili mema hivyo UWT kuwakusanya wasichana Wilayani Sengerema kwa ajili ya kuwafunza masuala mbalimbali yanayowahusu ni jambo jema ambalo litaleta tija na mabadiliko mema katika jamii.

Katika Kongamano hilo, wasichana zaidi ya Mia nane kutoka Vyuoni, Shule za Sekondari pamoja na majumbani kutoka Kata mbalimbali za Wilaya hiyo walipata fursa ya kufundishwa mada tofauti tofauti ambazo ni pamoja Historia ya Umoja wa Wanawake wa CCM, Kujitambua pamoja na Afya ya Uzazi ambapo pia Mtaturu aliwaasa wasichana hao kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.

Baadhi ya Wasichana waliopata fursa ya Kupokea kadi za Chama cha Mapinduzi walieleza kufurahishwa kwao na fursa waliyoipata ya kujiunga na Chama hicho lengo likiwa ni kuendelea kunufaika na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na chama hicho.
Wasichana waliohudhuria Kongamano la Wasichana Wilayani Sengerema wakinyoosha Miko juu kama ishara ya Kukubali kujiunga na Chama hicho.
Baadhi ya Wasichana waliopokea kadi za CCM wakila kiapo cha utii baada ya kupokea kadi hizo,
Katibu wa CCM Wilaya ya Sengerema Mohamed Shaban Mohamed (Alieshika Katiba ya CCM) akiwaapisha wasichana waliopokea kadi za Chama hicho (Hawapo pichani).
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akifungua Kongamano la Wasichana Wilayani Sengerema Ijumaa Iliyopita.
Baadhi ya Wasichana Wilayani Sengerema wakipokea Kadi za Chama cha Mapinduzi CCM.
Viongozi mbaimbali wa UWT Mkoa wa Mwanza wakiwa katika Kongamano la Wasichana Wilayani Sengerema Ijumaa iliyopita ambapo wa Kwanza Mushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Mama Maria Hewa (CCM).
Viongozi wa UWT SAUT wakiwa katika Kongamano hilo
Credit:Radio Metro

No comments:

Powered by Blogger.