UCHAMBUZI: UBINGWA LIGI KUU ENGLAND (EPL) UKO WAZI KWA CHELSEA.
0713208878
Ni siku chache zilizopita kwa wapenda soka ulimwengu kushuhudia mechi kati ya Chelsea na
Man united Binagi Media Group inakuletea kumbukumbu muhimu juu ya mechi hiyo.
Hii ni mechi ambayo ilipigwa katika dimba la Staford Bridge
kama ambavyo mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakiita uwanja huo kwa jina la
Darajani ikiwa ni mechi ambayo ilitarajiwa kuwa na upinzani mkubwa na mvuto wa
aina yake lakin haikuwa hivyo.
Kwa upande wa Chelsea ilikuwa ni mechi ya 701 tangu
inunuliwe na tajiri wa timu hiyo Roman Abramovich mwaka 2000 ambaye ametumia
paund million 916.95 kwa kipindi chote hicho.
Mechi hiyo ilichezwa majira ya saa 1.30 usiku kwa saa
zaAfrika Mashariki na zifuatazo ni takwimu za mechi 10 zilizopita kati ya
Chelsea na Man United.
2014/2015 Man united 1-1 Chelsea premier
2013/2014 Chelsea
fc 3-1 Man unit premier
2012/2013 Man unit 0- 0
Chelsea
premier
2012/2013 Man unit 0- 1 Chelsea
premier
2012/2013 Chelsea 5-4 Man unit league cup
2012/2013 Chelsea
2-3 Man unit premier
2011/2012 Chelsea 3-3 Man unit premier
2011/2012 Man unit 3-1 Chelsea
premier
2010/2011 Man unit 2-1 Chelsea
premier
2010/2011 Man unit 2-1 Chelsea
ligi ya mabingwa
Mechi 10 zilizopita
Man unit kashinda 4
Zote zimetoka Sare mara 3
MECHI ZA JUMLA
Man unit kashinda 68
Zimetoka Sare 50
Hizo ndizo takwim za timu hizi mbili ni mechi ambayo ilitakuwa
na upinzani wa aina yake kwani kwa kila timu point 3zilikuwa ni muhimu kwake japo kwa sasa Chelsea iko kileleni
mwa ligi ikiwa na point 76 ikiwa imecheza michezo 32 huku Man United ikiwa
nafas ya 3 na pointi zake 65 baada ya kushuka dimbani mara 33.
Nafasi ya 2 inashikiliwa na Asernal na point 66 akiwa
amecheza michezo 32 hata hivyo mambo yamebadilika baada ya timu za asernal na
man united kuzinduka toka usingizin na kuingia kwenye kundi la kupigania
ubingwa huku tukishuhudia Man City ikianza kupotea.
Kwa hali hii Chelsea anapewa nafasi ya kuchukua ubingwa
hivyo Mourinho hakuhitaji kucheza mchezo wa pasi bali alicheza mchezo wa kupaki
basi hivyo alichokuwa akiangalia ni point na siyo kucheza mchezo ambao ni show game kwan point 3 ni zilikuwa ni muhimu kwake na ndicho kitu alichokifanya huku
akiwa anajua kuwa ana kibarua kigum kwan mechi inayofuata ambapo atakuwa mdomon
mwa Asernal.
Lakin tukumbuke kuwa Mourinho ameishaweka kombe la Capital
one kabatini.Ni kwa nini nasema kuwa Chelsea alicheza mchezo mchafu usiyokuwa
na radha hilo lilionekana mapema toka siku Chelsea alipocheza mechi na QPR na Chelsea
aliibuka na ushindi wa goli 1-0 ambapo wasiwasi
wangu mkubwa kabla ya mechi hii ulikuwa ni kwa mabeki wa Man united ambao hata kwenye
mechi ya man United na Man City mabeki wa United walionekana kupwaya sana
hususani katika kipindi cha kwanza na kuwapatia nafasi mafowadi wa City kupata
nafasi lakini hawakuwa makini kutumia nafasi hizo.
Mechi hiyo ilionekana kuwa
ngumu kwa viungo wa Man united
kutokana na Chelsea kupaki basi katikati ya uwanja nikiwa namaanisha viungo ndo
wangeweza kuamua mchezo huo ila mwisho wa siku Chelsea iliibuka na ushindi
ambao ulikuwa ni muhimu kwao sare kwani hatamimi sikutarajia kama United ingeibuka na
ushindi darajani.Kwenye mchezo huo goli la Eden Hazard dakika ya 38 lilitosha
kuipa ushindi Chelsea licha ya Ushindi huo Man united walitawala mchezo mpaka
dakika 90 walikuwa wanaongoza umiliki wa mpira kwa 71% Kwa 19% za Chelsea.
Hata hivyo timu mbili hazikuwa na makeke ya kutosha na kila
moja ilipiga mashuti mawili tu
yaliyolenga lango kwa dakika zote 90.Mashuti ambayo hayakulenga langoMan
walipiga mashuti9 dhidi ya 3 ya Chelsea; United ilipata kona 7 dhidi 3
zaChelsea lakini United hawakukwepa kipigo toka kwa vinarahao wa ligi kuu
England hata hivyo ushindi huo umeifanya Chelsea kuwa mbele kw point kumi dhidi
ya mshindi wa pili ambaye ni Arsenal mwenye pointi 66
HIZI NI MECHI 6 ZILIZOBAKI CHELSEA KUWA BINGWA WA EPL
2014/2015.
Zimebaki mechi sita kwa Chelsea ili watangazwe kuwa mabingwa wa msimu
wa mwaka 2014/2015hadi kufikia tarehe 24 mwezi wa5 ndo tarehe ambayo
tutakuwa tumejuwa bingwa ni nani mechi
hizo ni;
Asrsenal Vs Chelsea [jumapili 26 /4]
LeicesterCity Vs Chelsea [jumatano 29/4]
Chelsea Vs Ceystal Palace[jumapili 3/5]
Chelsea Vs Liverpool[jumapili 10/5]
West Brownwich Abion Vs Chelsea [18/5]
Chelsea Vs Sundeland [24/4]
Kwa hali ilivyo ni matarajio ya wanamichezo wengi hata nami nikiwemo ya kwamba ni ukweli usiopingika kuwa Chelsea ndie bingwa wa Ligi Kuu Nchini Englind kwa Msimu wa mwaka 2014/15.
CREDIT:RADIO METRO
No comments: