LIVE STREAM ADS

Header Ads

TEMBO AWAHIMIZA MACHINGA JIJINI MWANZA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPATA VITAMBULISHO.

Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoani Said Tembo (Kulia) akiwa pamoja na Viongozi wengine wa Umoja huo ambao ni Mjumbe wa Muungano huo Concord Mbumbe (kushoto) pamoja na Amri Hamza (katikati) ambae ni Mwenyekiti wa Muungano huo Tawi la Igoma Jijini Mwanza.
Na: George GB Pazzo
Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza Said Tembo amewahimiza Wanachama wa Umoja huo kujisajili ili kupatiwa Vitambulisho vya Uanachama kwa lengo la kuondokana na Usumbufu unaoweza kuwakabili kutokana na kukosa vitambulisho.

Tembo ametoa Kauli hiyo hii leo Jijini Mwanza wakati akizungumza na Radio Metro juu ya zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogondogo katika Wilaya za Nyamagana na Ilemela.

Amesema kuwa kila mwanachama wa Umoja wa Machinga Mkoa wa Mwanza anapaswa kuwa na Kitambulisho hivyo mwanachama ambae atashindwa kujisajili na kupatiwa Kitambulisho hataweza kupata usaidizi wa aina yoyote pindi atakapopata tatizo la aina yoyote ile.

Amebainisha kuwa awali kulikuwa na ugumu kwa wanachama wa umoja huo kuweza kusaidiana katika masuala mbalimbali hivyo Vitambulisho hivyo ni muhimu kwa kila mwanzachama kwa kuwa vitaweza kuwasaidia wanachama kupata msaada wakati wa matatizo ama dharura pamoja na kuwatambulika wanachama wa Muungano huo katika taasisi mbalimbali zikiwemo taasisi za kifedha.

Aidha Tembo amefafanua kuwa gharama kwa kila mwanachama anaehitaji kupata kitambulisho ni shilingi elfu Tano huku akibainisha kuwa zoezi za ugawaji wa Vitambulisho hivyo kwa sasa linatekelezwa katika Wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela kabla ya kuhamia katika Wilaya nyingine za Mkoa wa Mwanza.

Nae Amri Hamza ambae ni Mwenyekiti wa Umoja wa Machinga Tawi la Igoma Jijini Mwanza amesisitiza kuwa Vitambulisho hivyo ni muhimu kwa kila Machinga Mkoani Mwanza kwa kuwa vitaweza kumtambulisha mwanachama pindi atakapokuwa anahitaji msaada popote pale atakapokuwa ndani na nje ya Mkoa wa Mwanza.

Kwa upande wao baadhi ya Wanachama wa Muungano wa Machinga Mkoani Mwanza wameelezea kulipokea vyema zoezi hilo la kupatiwa Vitambulisho, ambapo wameupongeza Uongozi wa wa Muungano huo kwa zoezi hilo huku wakiongeza kuwa kwa hivi sasa Machinga Mkoani Mwanza wanafanya biashara zao katika hali ya utulivu bila buguza za aina yoyote ikiwa ni ushirikiano wa pamoja baina ya uongozi wao na Viongozi wa Serikali katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoani Said Tembo (Kulia) akiwa pamoja na Viongozi wengine wa Umoja huo ambao ni Mjumbe wa Muungano huo Concord Mbumbe (katikati) pamoja na Amri Hamza (kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Muungano huo Tawi la Igoma Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoani Said Tembo (Kushoto) akiwa pamoja na Viongozi wengine wa Umoja huo ambao ni Mjumbe wa Muungano huo Concord Mbumbe (katikati) pamoja na Amri Hamza (wa tatu kutoka kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Muungano huo Tawi la Igoma Jijini Mwanza. Wa kwanza kulia ni Maneno Juma ambae ni Muuzaji wa Banda hili.
Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoani Said Tembo (Kulia) akiwa pamoja na Viongozi wengine wa Umoja huo ambao ni Mjumbe wa Muungano huo Concord Mbumbe (mwenye nguo nyekunduku) pamoja na Amri Hamza (wa pili kulia) ambae ni Mwenyekiti wa Muungano huo Tawi la Igoma Jijini Mwanza. Wa tatu kulia ni Lugaila Malele ambae ni machinga na wa kwanza kushoto waliokaa ni Bi.Hidaya Juma.
                                                 CREDIT: RADIO METRO

No comments:

Powered by Blogger.