LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTATURU AHIMIZA KUSITISHWA SHUGHULI ZA UZALISHAJI KATIKA HIFADHI YA SAYAKA NA BONDE LA BUBINZA WILAYANI MAGU.

Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ikiwa katika Hifadhi ya Sayaka Wilayani Magu wiki iliyopita.
Na:George GB Pazzo
Wananchi Wilayani Magu Mkoani Mwanza wametakiwa kufuata sheria na taratibu za nchini na hivyo kusitisha shughuli zao za Uzalishaji na Makazi katika maeneo ya Hifadhi ya Sayaka pamoja na Bonde la Bubinza Wilayani humo.

Rai hiyo ilitolewa wiki iliyopita na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu, alipotembelea maeneo hayo ambayo yamekuwa yakiibua migogoro baina ya wananchi na Serikali alipokuwa katika ziara yake ya Siku mbili Wilayani Magu.

Aliwataka wananchi hao kusitisha shughuli zote ambazo ni Makazi, Kilimo pamoja Ufugali katika eneo la Hifadhi ya Sayaka kwa kuwa eneo hilo limeelewa kuwa eneo pekee katika Mkoa wa Mwanza ambalo linasaidia mabadiliko ya tabianchi huku bonde la Bubinza likielezwa kuwa eneo la mazalia mazuri ya samaki.

Aidha aliwaonya baadhi ya wanasiasa na viongozi ambao wamekuwa wakiwapotosha wananchi kuwa watawasaidia katika kubadilisha matumizi ya eneo hilo la Sayaka ambalo lilitengwa na Serikali kuwa Hifadhi tangu mwaka 1996.

Julius Maira ambae ni Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Wilayani Magu alisema kuwa awali eneo hilo la Hifadhi ya Sayaka lenye Hekta Eflu tano mia nne lilikuwa ni msitu wa asili lakini kutokana na Shughuli za binadamu eneo hilo limeharibiwa vibaya na hivyo kuhatarisha uoto wa asili.

Wananchi wa wanaoishi katika maeneo jirani na Hifadhi hiyo ya Sayaka pamoja na Bubiza walieleza kusikitishwa na maamuzi yaliyotelewa na Serikali ya kuwataka kusitisha shughuli zao katika maeneo hayo kwa kuwa hawakushirikishwa ipaswavyo juu ya wao kuondoka katika maeneo hayo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) akizungumza alipotembelea Hifadhi ya Sayaka ambayo iko hatarini kutoweka kutokana na shughuli za Kibinadamu.
Julius Maira (Kushoto) ambae ni Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Wilayani Magu akitoa taarifa mbele ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kulia) alipotembelea Hifadhi ya Msitu wa Sayaka Wilayani Magu wiki iliyopita. Katikati ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mayunga Mangelepa (Me) akifuatiwa na Dinah Samani (Ke) ambae ni Katibu wa Wazazi CCM Mkoa wa Mwanza.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Ntinika William Paul akitoa Ufafanuzi wa Maswali ya Wananchi katika ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu iliyotembelea Hifadhi ya Sayaka Wilayani Magu wiki iliyopita.
Bashir Muhoja ambae ni Mwanzasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Bubinza Wilayani Magu lilipo Bonde la Bubinza akizungumza wakati wa Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza katika Ziara ya Kutembelea Hifadhi ya Sayaka pamoja na Bonde la Bubinza wiki iliyopita.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Bubinza Wilayani Magu lilipo Bonde la Bubinza akizungumza wakati wa Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza katika Ziara ya Kutembelea Hifadhi ya Sayaka pamoja na Bonde la Bubinza wiki iliyopita.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Sayaka Wilayani Magu ilipo hifadhi ya Sayaka akizungumza wakati wa Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza katika Ziara ya Kutembelea Hifadhi ya Sayaka pamoja na Bonde la Bubinza wiki iliyopita.
Baadhi ya wananchi wa Vijiji vya Bubinza na Sayaka wakimsikiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza (Hayuko pichani) alipotembelea hifadhi ya Sayaka na Bonde la Bubinza wiki iliyopita.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu ikikagua Mashine ya Kusukuma Maji kutoka katika Chanzo cha Maji kilichopo Kijiji cha Bugabu Kata ya Kahangara Wilayani Magu alipokuwa katika ziara yake Wiki iliyopita.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye Kofia) ikikagua Mashine ya Kusukuma Maji kutoka katika Chanzo cha Maji kilichopo Kijiji cha Bugabu Kata ya Kahangara Wilayani Magu alipokuwa katika ziara yake Wiki iliyopita.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akishiriki katika Ujenzi wa Choo cha Shule ya Msingi Moha Wilayani Magu alipotembelea Ujenzi wa Majengo Mapya ya Shule hiyo Wiki iliyopita ambapo kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza aliahidi kutoa Mifuko 20 ya Simenti kwa ajili ya kusaidia katika Ujenzi wa Shule hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye kofia) pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali Wilayani Magu akishiriki katika Ujenzi wa Choo cha Shule ya Msingi Moha Wilayani Magu alipotembelea Ujenzi wa Majengo Mapya ya Shule hiyo Wiki iliyopita ambapo kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza aliahidi kutoa Mifuko 20 ya Simenti kwa ajili ya kusaidia katika Ujenzi wa Shule hiyo.
Jengo jipya la Shule ya Msingi Moha Wilayani Magu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akiwa pamoja na Viongozi wengine wa Chama na Serikali katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Sabasaba Wilayani Magu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi wa Magu katika Mkutano wa hadhara uliofanyika wiki iliyopita katika Uwanja wa Sabasaba Wilayani Magu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kulia) akizungumza na wananchi wa Magu katika Mkutano wa hadhara uliofanyika wiki iliyopita katika Uwanja wa Sabasaba Wilayani Magu ambapo kushoto ni Mhandisi Joseph Bundala ambae ni Meneja Mamlaka ya Maji Wilayani Magu akitoa ufafanuzi wa lini tatizo la Maji litaisha Wilayani Magu ambapo aliahidi kuwa tatizo hilo linashughulikiwa na muda si mrefu litakuwa limetatuliwa.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mayunga Mangelepa akitoa salamu zake katika Mkutano wa hadhara uliofanyika wiki iliyopita Wilayani Magu katika Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza.
Wananchi na Wanachama wa CCM wakimsikiliza kwa Makini Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu katika Mkutano wa hadhara uliofanyika wiki iliyopita Wilayani Magu.
Wananchi na Makada wa CCM wakinyoosha Mikono juu kushangilia maneno kuntu ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (hayuko pichani) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Wiki iliyopita WIlayani Magu.
SOURCE: RADIO METRO FM

No comments:

Powered by Blogger.