TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWAO JERUSALEM CITY SINGERS MWANZA.
Na:George GB Pazzo
Baada ya Kukamilika kwa utengenezaji wa Video ya albamu yao ya pili inayokwenda kwa jina la HAJAKUSAHAU, Kwaya ya ya Muziki wa Injili JERUSALEM CITY SINGER kutoka Bugarika Jijini Mwanza imetangaza tarehe rasmi ya uzinduzi wa Albumu hiyo.
Akizungumza na Binagi Media Group mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kwaya hiyo Samwel Maneno alisema kuwa albamu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa jumapili ya tarehe 10 mwezi wa Tano Mwaka huu (10/05/2015) katika Ukumbi wa Coconut Hotel Jijini Mwanza.
Maneno alisema kuwa Albamu hiyo imerekodiwa kwa kiwango na ubora wa hali ya juu hivyo ni vyema kila mmoja akahakikisha kuwa anajipatia nakala yake ambapo pia alitoa rai kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa Albamu hiyo ambao pamoja na Jerusalem City Singer kutumbuiza pia Waimbaji na Kwaya mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Mwanza zitakuwepo.
Alisema kuwa katika Uzinduzi huo hakutakuwa na kiingilio hivyo kila mmoja atapata fursa ya kushuhudia albamu hiyo inavyozinduliwa huku akibainisha kuwa watakaofika katika uzinduzi wa albamu hiyo watajipatia nakala yake kwa gharama nafuu kabisa.
Mgeni rasmi katika Uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Robert Masunya ambae ni Afisa Uhusiano kutoka Mamlaka ya Maji Taka na Maji Safi Mkoani Mwanza MWAUASA ambae pia ni Kamanda wa Umoja wa Vijana UVCCM Kata ya Butimba Jijini Mwanza.
Albamu hiyo imesheheni nyimbo kumi bora ambazo ni Tembea na Yesu, Nikupe Habari, Hajakusahau (wimbo uliyobeba jina la Albamu), Hii ndiyo habari, Ahsante, Nyakati za Hatari, Utatu Mtakatifu, Mungu wa Ajabu, Ilisikika Sauti pamoja na Kwa Rehema za Mungu.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA "HAJAKUSAHAU" KUTOKA KWAO JERUSALEM CITY SINGERS. MAWASILIANO-0758 061 044 au 0763 185 898
BINAGI MEDIA GROUP PRODUCTION-O757 43 26 94
No comments: