LIVE STREAM ADS

Header Ads

BASI LA BUNDA EXPRESS LAPINDUKA JIJINI MWANZA.

Picha kutoka Maktaba
ELISA ANATORY/ 0763345064
EMAIL anatoryelisa@gmail.com

Watu wanne wamejeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea jana katika eneo la Tanesco barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi na moja za alfajiri ikihusisha basi la Bunda express lenye namba za usajili T 318 CXZ linalofanya safari za Mwanza kwenda Bukoba Mkoani Kagera ambapo lilikuwa likitokea Kituo Cha Mabasi Buzuruga kuelekea Kituo cha Mabasi Nyegezi ambapo.

Chanzo cha ajali hiyo ni baada ya dereva kushindwa kukwepa gari la kushindilia barabara lililokuwa limepaki katika Barabara  Kenyata eneo la eneo la Tanesco ambapo kuna matengenezo ya barabara.

Dakitari wa  zamu wa hospitali ya Rufaa ya Bugando ambapo majeruhi hao walipelekwa Edwini Mbwambo aliwataja majerui hao kuwa ni Alfan Yusufu (50),Christian Iyakugilwa (65), Richard Malema (30) pamoja Valentine Kalamagangara (30)

Baadhi ya Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi hilo alishindwa kulimudu na hatimae kugonga gari la kushindilia barabara na hatimae kupinduka.

Hadi tunakwenda mitamboni, Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza alikuwa hajapatikana ili kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.