HII NDIYO KAULI YA SHILLATU KWA WATANZANIA DHIDI YA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Tatu ya Kidato cha Sita katika shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza Raphael Shilatu (katikati ya Wanafunzi) akiwakabidhi wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaosoma shuleni hapo Fedha kiasi cha Shilingi Laki Moja na Elfu Thelani na Tano (135,000) alizozichanga kwa kushirikiana na wageni waalikwa, waalimu na wanafunzi kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi hao katika mahitaji yao. Aliesimama kushoto ni mwalimu wa wanafunzi hao wa Lugha ya ishara (Kwa wasiosikia).
Na:George GB Pazzo
Jamii ya Watanzania imetakiwa kuacha Imani
potofu ya Kuhusisha Mafanikio ya aina yoyote ile na Viungo vya Watu wenye Ulemavu
wa Ngozi, badala yake ijitoe kwa hali na mali katika kuwalinda watu hao.
Kauli hiyo ilitolea ijumaa iliyopita
na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Raphael Shillatu, ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya tatu ya Kidato cha Sita katika Shule ya
Sekondari Mkolani iliyopo Kata ya Mkolani Jijini Mwanza.
Shillatu alisema kuwa anasikitika
kuona kila siku Watanzania wenye Ulemavu wa ngozi wanapoteza Viuongo vyao huku
wengine wakipoteza maisha yao kutokana na baadhi ya Watanzania kuhusisha viuongo
vya Watu wenye ulemavu wa ngozi na mafanikio yao mbalimbali.
“Vitu vya Kijinga sana, vitu vya
kipuuzi sana, vitu ambavyo havina tija wala uhusiano hata kidogo na Utajiri, udiwani,
ubunge, Uwaziri wala Urais na ndiyo maana tunaendelea kukemea tabia hii ya
kuwakata na kuwadhuru binadamu wenzetu wenye ulemavu wa ngozi”. Alisema
Shillatu huku akiwataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ikiwa wanahitaji
kufikia mafanikio yao.
Shillatu aliyasema hayo huku
akiwahimiza Wazazi na wageni waalikwa waliokuwa wamealikwa katika Mahafali hayo
kuwachangia pesa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaosoma katika Shule hiyo
ya Mkolani Sekondari kwa ajili ya mahitaji yao ambapo takribani Shilingi Laki
Moja na Elfu Thelathini na Tano (135,000) ziliweza kupatikana huku pia
akichangia Mifuko 10 ya theluji kwa ajili ya kusaidia katika ujenzi wa darasa
unaotarajia kuanza wiki hii kwa fedha za michango ya wazazi.
Takribani watu 43 wenye ulemavu wa
ngozi wameweza kuuawa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa katika Kipindi cha Mwaka
2005 hadi mwaka huu huku wengine wakijeruhiwa na kupoteza viungo mbalimbali vya
miili yao ambapo imani potofu za kuhusisha viungo vya watu hao na Mafanikio ya
Utajiri na Vyeo mbalimbali imekuwa ikihusishwa katika Ukatili huo, jambo ambalo
halina ukweli wowote na wananchi wamekuwa wakihimizwa kuachana na imani hiyo na
hivyo kushiriki katika kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi kote nchini.
Akizungumza katika Mahafali hayo, Mkuu
wa Shule ya Sekondari Mkolani Asensio Mathias aliwapongeza wahitimu wote kutokana
na bidii ya kujisomea pamoja na nidhamu waliyoinyosha katika kipindi cha masomo
yao huku akibainisha kuwa Morali ya Usomaji kwa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza
hadi cha Nne shuleni hapo imepungungua na hivyo kuwasihi wanafunzi wa vidato
hivyo kuongeza juhudi katika kujisomea.
Jumla ya Wanafunzi 53 ambao wa Kike ni
48 na wa kiume Watano waliojiunga na Kidato cha Tano mwezi July mwaka 2013
katika Shule hiyo ya Mkolani Sekondari wamehitimu masomo yao katika Michepuo ya
Sayansi ambayo ni PCM, PCB na CBG ambapo wamewahisi wanafunzi hususani wa Kike
hapa nchini kupenda kusoma masomo ya Sayansi na kuachana na utamaduni
uliozoeleka kwamba Masomo hayo ni Magumu.
No comments: