LIVE STREAM ADS

Header Ads

NI BONGE MOJA LA BURUDANI KATIKA SHOW YA JEMBEKA FESTIVAL...WASIKILIZE JJ BAND HAPA.

Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa, ile band ambayo kwa walio mbali basi walikuwa wakisikia simulizi zake toka kwa wenyeji kwamba inafumua burudani ya kijanja ile kisawasawa toka kiota chenye hadhi ya kitalii Jembe Beach Resort Mwanza, JJ Band ndiyo ninao wazungumzia, basi wamekuja na single yao ya kwanza mpya inayoitwa 'NISHIKE'

Kazi imefanyika ndani ya studio za One Love FX zilizoko Ilemela jijini Mwanza, chini ya mkono wa mtayarishaji mkali Tiddy Hotter, yule aliye tengeneza ngoma kama Changamka ya Director Shahib, Tumewaka - G Nako ft Godzillah, Mimi na wewe - Dynna Nyange, Listen - Belle Nine, Itika - Josline na nyingine kali kibao.

Kazi tamu kwa sikio, yenye hisia na inayochezeka bado mbichi kabisa isikilize kwa nafasi ikiwa ni amsha amsha ya kuelekea tarehe 23 May 2015 ambapo barabara zote za jiji la Mwanza zitaelekea CCM Kirumba katika tamasha kubwa la burudani 'JEMBEKA FESTIVAL 2015' OYOMBA YES - PAMOJA SANA 

No comments:

Powered by Blogger.