KATIBU WA BAWACHA KATA YA BUTIMBA JIJINI MWANZA AWASHAURI WANAWAKE NCHINI.
Veronica Method Tuhuye ambae ni Katibu Mwenezi BAWACHA Kata ya Butimba Jijini Mwanza
Na:Binagi Media Group
Wanawake nchini wameshauriwa
kushiriki katika Shughuli mbalimbali za Kimaendeleo zinazowazunguka na hivyo
kuachana na misingi ya Kubweteka kutokana na Mazoea na dhana ya Kusubiri
kuwezeshwa.
Rai hiyo ilitolewa
jana na Veronica Method Tuhuye ambae ni Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA (BAWACHA) Kata ya Butimba Jijini Mwanza,
wakati akizungumzia nafasi ya Mwanamke ndani ya Chadema katika kuwania nafasi
mbalimbali za Uongozi.
Tuhuye alisema
kuwa ndani ya Chadema wanawake wanapata fursa mbalimbali za Kuwania nafasi za
Uongozi ambapo jambo kubwa lililopo ni wanawake wenyewe kujiamini na kujitokeza
kwa wingi katika kuwania nafasi hizo.
Aidha Tuhuye
aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika Mkutano wa Hadhara
unaotarajiwa kufanyika Wiki hii katika Kata yake ya Butimba, Mkutano ambao
utafanyika siku ya Alhamisi ya May 21
katika Uwanja Butimba Sokoni ambapo mzungumzaji Mkuu anatarajiwa kuwa Mbunge wa
Jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje (Chadema).
Katika hatua
nyingine Tuhuye ambae alijiunga na Chadema tangu Mwezi Januari mwaka huu akitokea
CCM, alibainisha kuwa ndani ya Chadema kuna jukumu moja tu la kuwatumikia
Watanzania bila kujali kujuana tofauti na CCM ambapo hali ni tofauti na kwamba
nafasi za uongozi zinatolewa kwa kujuana.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
Veronica Method Tuhuye ambae ni Katibu Mwenezi BAWACHA Kata ya Butimba Jijini Mwanza
Veronica Method Tuhuye ambae ni Katibu Mwenezi BAWACHA Kata ya Butimba Jijini Mwanza
Veronica Method Tuhuye ambae ni Katibu Mwenezi BAWACHA Kata ya Butimba Jijini Mwanza akizungumza nasi.
No comments: