KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA MIRAJI MTATURU AWAFUNZA VIONGOZI WA KISIASA NCHINI.
Miraji Mtaturu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza
Viongozi
wa vyama vya siasa nchini wametakiwa kuwatumikia wananchi bila kujali itikadi
za aina yoyote hususani za kisiasa, ili kuendelelea kuidumisha
amani iliyopo hapa nchini.
Kauli hiyo ilitolewa Jumamosi
iliyopita na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu,
katika mkutano wa hadhara wa chama hicho, uliofanyika Kata ya Pansiasi
Wilayani Ilemela.
Mtaturu alisema kuwa wapo baadhi
ya viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini ambao wanawatumikia wananchi kwa
ubaguzi wa itikadi za vyama vyao hivyo ni vyema wakaepukana na tabia hiyo ili
amani iendelee kudumu nchini.
“Nawaombeni viongozi wa vyama vya
siasa, watumikieni wananchi bila kujali itikadi za aina yoyote ikiwemo za kisiasa,
kwani mkiwabagua amani haiwezi kuwepo nchini”. Alisema Mtaturu.
Hata hivyo alisema kuwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kitaendelea kuwatumikia wananchi kwa kuwapatia huduma
mbalimbali za Kimaendeleo bila kujali maeneo wanayoishi yanaongozwa na CCM au
chama kingine cha Kisiasa.
“CCM itaendelea kuwaletea huduma
mbalimbali bila kujali eneo mnaloishi linaongozwa na chama gani”. Alisema.
Naye Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa
Mwanza Simon Mangelepa alisema kuwa msingi mkubwa wa amani kuwa ni haki hivyo viongozi
wa Kisiasa wanapowanyima haki wananchi wanaweza kusababisha vurugu kutokea
na hatimae kusababisha kupotea kwa amani nchini.
No comments: