TAIFA STARS YATHIBITISHA USEMI USEMAO SOKA LA BONGO NI SAWA NA KICHWA CHA MWENDA WA ZIMU.
Na:Genya Richard
Timu ya Taifa ya Taifa Stars imeanza vibaya michuano ya kombe la
COSAFA baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Swaziland katika mchezo
wa kwanza wa kundi B uliopigwa uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace.
Matokeo hayo yanaiweka pabaya Stars inayofundishwa na Mholanzi
Mart Nooij katika mazingira magumu ya kwenda robo fainali baada ya Madagascar
kuifunga 2-1 Lesotho katika mchezo wa kwanza.
Stars sasa lazima ishinde mechi zake mbili zijazo dhidi ya Lesotho
na Madagascar ili kuangalia uwezekano wa kwenda Robo Fainali .
Katika mchezo wa jana uliochezeshwana refa Nelson Emile Fred wa
Shelisheli ambapo alisaidiwa na Akhtar Nawaz Rossaye wa Mauritius na Isaskar
Boois wa Namibia, hadi mapumziko tayari Swaziland walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na Sifiso Mabila kwa shuti kali dakika ya 42
baada ya kutanguliziwa pasi kwenye njia sahihi na mchezaji Xolani Sibandze
aliyemtoka Oscar Joshua upande wa kushoto.
Taifa Stars ilitengeneza nafasi tatu nzuri kipindi cha kwanza
ambazo kwa bahati mbaya hazikuzaa matunda ambapo Simon Msuva alishindwa
kuzitumia na John Bocco alipoteza nafasi moja.
Kipindi cha pili Swaziland walitawala zaidi mchezo lakini safu ya
ulinzi ya Stars ilikuwa imara kutoruhusu bao jingine.
Nafasi pekee nzuri ambayo Stars waliipata ilikuwa ni kipindi cha
pili katika dakika ya 65 baada ya Said Ndemla kupiga shuti juu ya lango akiwa
ndani ya boksi kufuatia pasi nzuri ya John Bocco.
Swaziland waliizidisha ufundi uwanjani na kutawala mchezo huo
ambapo walimiliki mpira kwa asilimia 54 kwa 46 dhidi ya Stars.
Naye Tony Tsabedze alitajwa mchezaji bora wa mechi baada ya mchezo
huo.
Kikosi cha Stars kilikuwa kama ifuatavyo; Deo Munish, Shomari
Kapombe, Oscar Joshua;Salum Mbonde; Aggrey Moris;ErastoNyoni;Mrisho
Ngassa/Salum Abubakar dak75;Mwinyi Kazimoto;John Bocco;Said Ndemla/Juma Luizio
dk65;na Saimon Msuva/Ibrahim Hajibu dk 67
Nao Watanzania waishio miji mbalimbali Afrika Kusini walijitokeza
kwa wingi katika uwanja huo wa Royal Bafokeng Sport Palace kuishangilia Taifa
Stars ambapo walishuhudia timu yao ikipewa kichapo cha bao 1-0
Pia wapo waliokuja kutoka Johannesburg na bango lenye picha ya
baba wa Taifa , marehem Mwalimu Julius Nyerere lisemalo WANADAMU WOTE NI NDUGU
NA AFRIKA MOJA.
Mimi nasema "Kweli soka letu ni kichwa cha mwenda wa zimu maana kila michuano
tunayoshirki tumekuwa ni wasindikizaji ila Watanzania nawasihi tuwe wavumilivu
ipo siku na sisi tutapata matokeo mazuri tutajiandaa vyema".
No comments: