TIGO NA HUAWEI WATOA MSAADA WA KOMPYUTA 25 HOSPITAL YA MKOA WA MWANZA SEKOUR TOURE.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisana (Kulia) akipokea Msaada wa Kompyuta 25 zenye Huduma ya Internet ya Bure bila Kikomo zilizotolewa na Kampuni za Tigo na Huawei katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure jana. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini Diego
Gutierrez.
Na:George GB Pazzo
Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure
inatarajia kuboresha huduma zake za utunzaji wa kumbukumbu za Wagonjwa na Mapato, baada ya kupokea msaada wa Kompyuta
25 zilizotolewa na Kampyuni za Tigo na Huawei.
Hayo yalielezwa jana na Onesmo Rwakyendera
ambae ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, wakazi wa zoezi la utoaji wa Kompyuta
hizo lililofanyika hospitalini hapo.
Rwekyendera alibainisha kuwa awali
hospitali hiyo ilikuwa ikitunza Kumbukumbu za Wagonjwa na Mapato katika Mfumo
wa Makaratasi, jambo ambalo lilikuwa likisababisha ugumu na Usumbufu mkubwa katika
utendaji wa kazi.
Aliutaja ugumu huo kuwa ni Kumbukumbu
za wagonjwa kutopatikana kwa wakati pindi zinapohitajika kutokana na wingi wa
Mafaili ya Wagonjwa hospitalini hapo, pamoja na upotevu wa Mapato kutokana na
mkanganyiko wa taarifa zinazoandikwa kwenye karatasi.
“Tuna imani kuwa vifaa hivi
vitatupatia taarifa kamili za mapato na matumizi ya kila siku, ambapo pia
vitatupatia taarifa juu ya yale yanayoendelea katika ulimwengu wa matibabu
ikiwa ni pamoja na utafiti na masomo kutoka maeneo mbalimbali”. Alisema
Rwekyendera.
Ally Maswanya ambae ni Meneja wa Kampuni
ya Tigo Kanda ya Ziwa alibainisha kuwa Komputa zilizotolewa hospitalini hapo zina
thamani ya takribani Shilingi Milioni Thelathini ambapo zitakuwa na huduma ya Intaneti
ya Bure bila Kikomo, huku akilitaja lengo la msaada huo ni kuhakikisha kuwa
Utunzaji wa Kumbukumbu unaboreshwa zaidi hospitalini hapo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza, Baraka Konisaga ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana alibainisha
kuwa Serikali inatambua mchango wa Sekta binafsi hapa nchini katika kuboresha
huduma za Kijamii huku akiongeza kuwa Msaada wa Kompyuta uliotolewa na Kampuni
za Tigo na Huawei unaunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza mpango
wake wa Afya wa Mwaka 2013/18 ambao umelenga kuhakikisha kuwa huduma za Afya zinaingia
katika mifumo ya Kidijitali.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini
Diego Gutierrez alisema kuwa Msaada uliotolewa na katika Hospitali ya Sekour
Toure ni katika Kutekeleza Mkakati wa Kampuni hiyo wa Kuyabadilisha maisha ya
Watanzania katika sekta mbalimbali ambazo ni pamoja na Afya kuwa katika Mfumo wa
Kidijitali.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Huawei
Zhang Yongquan alisema kuwa msaada huo wa Komputa unaonyesha jinsi ambavyo
Kampuni yake imejitolea katika Kusaidia Sekta ya Afya nchini ili kuendana na
Mabadiliko ya Kiteknolojia.
Mwenyekiti wa Bodi wa Hospitali hiyo
ya Sekour Toure Christopher Mwita Gachuma, alitoa rai kwa uongozi wa Hospitali
hiyo kuhakikisha kwamba Komputa zilizotolewa na Kapuni za Tigo na Huawei
zinatunzwa vizuri pamoja na zizitumia kwa ajili ya matumizi yaliyokusudiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Wa pili kulia) akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Onesmo Rwakyendera (Mwenye Koti Jeupe) ikiwa ni msaada uliotolewa na Kampuni za Tigo na Huawei.
Kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini Diego
Gutierrez, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Hospitali ya Sekour
Toure Christopher Mwita Gachuma, anaefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu), akifuatiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Huawei Zhang Yongquan na wa mwisho ni Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure Onesmo Rwakyendera.
Kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini Diego Gutierrez, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Hospitali ya Sekour Toure Christopher Mwita Gachuma
Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa Ally Maswanya (Mwenye koti) akiwa na Wafanyakazi wengine wa Kampuni hiyo.
Wafanyakazi wa Tigo
Wafanyakazi wa Tigo na Huawei
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure
Watumishi wa Sekour Toure
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu)
Neno kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (Mwenye kinasa sauti).
Neno kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini Diego
Gutierrez (mwenye kinasa sauti).
Mwenyekiti wa Bodi wa Hospitali hiyo ya Sekour
Toure Christopher Mwita Gachuma
Onesmo Rwekyendera ambae ni Kaimu Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Huawei Zhang Yongquan
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini Diego
Gutierrez
Ze Kompyutaz zilizotolewa na Kampuni za Tigo na Huawei
Picha ya Pamoja.
Special Thanks to Our Reader Nelson The Only One.
No comments: