LIVE STREAM ADS

Header Ads

PUMZIKA KWA AMANI MTOTO HAPPINESS ZEPHANIA MANG'ACHE...DAIMA TUTAKUKUMBUKA MILELE.

Sara ya Mazishi ya Mtoto HAPPINESS ZEPHANIA MANG'ACHE (08) Mkazi na Mzaliwa wa Kijiji cha Kenyamanyori Wilaya ya Tarime Mkoani Mara ikifanyika Kijijini kwao Juzi Jumatano May 20, 2015. 
Mtoto HAPPINESS alifariki dunia Jumanne Usiku May 19, 2015 katika Hospital ya Tarime Goodwill Foundation (Kwa Winani) baada ya kuugua kwa muda akisumbuliwa na Maradhi ya Figo na Moyo. Mtoto Happiness alikuwa ni Mwanafunzi wa darasa la Pili katika Shule ya Msingi Kenyamanyori. Hakika Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe, AMEN!
Na: BINAGI MEDIA GROUP
Mtoto Happiness Zephania Mang'ache (08) akipumzishwa katika nyumba yake ya Milele
Baba wa Happiness (Anaeshika udongo) akimuaga mwanae katika safari yake ya kuishi hapa duniani
Wananzengo wakishiriki Mazishi
Binagi Mang'ache ambae ni Baba mdogo wa Happness akitoa Shukrani kwa walioshiriki mazishi...Kulia ni baba mzazi wa Happiness.
Mwalimu John Onditi (Mwenye Kinasa Sauti) ambae ni Mwalimu wa Darasa wa Happness aliekuwa akisoma darasa la Pili katika Shule ya Msingi Kenyamanyori.
Andiko kwa ajili ya Sara ya Marehemu likisomwa!
Kutoka Kushoto ni Baba Mzazi wa Mtoto Happy Zephania Mwita Mang'ache akifuatiwa na Mama Mzazi wa Happy Mbawazi Mwita Mang'ache..Wanaofuata ni Baba na Mama mdogo wa Happy na wa mwisho Kulia ni Babu wa Happy.
Wanazengo wakiwa Msibani
Wanafunzi wa darasa la Pili Shule ya Msingi Kenyamanyori wakimuaga HAPPINESS MWITA MANG'ACHE ambae alikuwa ni mwanafunzi mwenzao alietangulia mbele za haki.
Waalimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kenyamanyori wakiuaga mwili wa mtoto Happy
Wanafunzi waliokuwa wakisoma na Mtoto HAPPINES MWITA MANG'ACHE pamoja na Waalimu wao wakiwa katika picha ya pamoja.
PUMZIKA KWA AMANI MTOTO HAPPINESS MWITA MANG'ACHE (08) JAPO UMEONDOKA MAPEMA SANA...HAKIKA KAZI YA MOLA HAINA MAKOSA...DAIMA TUTAKUKUMBUKA.

No comments:

Powered by Blogger.