LIVE STREAM ADS

Header Ads

KONISAGA AZISHAURI TAASISI BINAFSI NCHINI KUACHA MARUMBANO NA SERIKALI NA KUFUATA NYAYO ZA TCCIA.

Kutoka Kushoto ni Joseph Kahungwa ambae ni Makamu wa Rais TCCIA, akifuatiwa na Julius Kaijage ambae ni Makamu Mwenyekiti Biashara kutoka TCCIA, anaefuata ni Eng.Peter Chisawillo ambae ni Rais wa TCCIA Taifa, akifuatiwa na Yakub Hasham ambae ni Makamu Mwenyekiti Viwanda kutoka TCCIA na wa Mwisho ni Daniel Machemba ambae ni Mkurugenzi Mtendaji TCCIA.
Na:George GB Pazzo
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga
Taasisi mbalimbali kutoka Sekta binasi hapa nchini zimeshauriwa kuacha Marumbano dhidi ya Serikali, badala yake ziendelee kuimarisha uhusiano uliopo baina yake na Serikali.

Kauli hiyo ilitolewa jana Jijini Mwanza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA.

Konisaga ambae ni maarufu kwa jina la Mtumishi wa Mungu, alisema kuwa muda wa Taasisi binafsi kuendelea kurumbana na Serikali umepitwa na wakati hivyo ni vyema Taasisi hizo zikatumia meza ya mazungumzo katika kutatua changamoto mbalimbali pindi zinapojitokeza.

Alisema kuwa baadhi ya Taasisi zimekuwa zikirumbana na Serikali hadi kufikia hatua ya Kuandamana isivyo sahihi hivyo ni vyema Taasisi za aina hiyo zikaiga mfano kutoka TCCIA ambayo imekuwa ikitumia meza ya mazungumzo katika kutatua changamoto zake.

"Serikali ina changamoto zake lakini pia Sekta binafsi zina changamoto zake hivyo nashauri ni vyema kila wakati tukawa tukutana kwa lengo la kujadili na kuzitatua changamoto hizo, badala ya kuendeleza marumbano yasiyo na tija".Alisema Konisaga huku akiongeza kuwa Serikali iko tayari kuendeleza Ushirikiano na Sekta binafsi kwani sekta binasi ni mhimili mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Katika hatua nyingine Konisaga alitumia fursa ya Mkutano huo kuihimiza TCCIA kusaidia katika Kuvitangaza Vivutio vilivyopo Mkoani Mwanza, kwa ajili ya Kusaidia kukuza sekta ya Utalii na hivyo kuinua Uchumi kupitia Sekta hiyo.

Makamu wa Rais wa TCCIA Joseph Kahungwa aliipongeza Serikali kwa namna ambavyo imeendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya biashara ambapo alitoa rai changamoto hizo kuendelea kutatuliwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa Miundombinu ya barabara na Reli ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa.
Kutoka Kushoto ni Joseph Kahungwa ambae ni Makamu wa Rais TCCIA, akifuatiwa na Julius Kaijage ambae ni Makamu Mwenyekiti Biashara kutoka TCCIA, anaefuata ni Eng.Peter Chisawillo ambae ni Rais wa TCCIA Taifa, akifuatiwa na Yakub Hasham ambae ni Makamu Mwenyekiti Viwanda kutoka TCCIA na wa Mwisho ni Daniel Machemba ambae ni Mkurugenzi Mtendaji TCCIA.
TCCIA
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TCCIA Taifa uliofanyika Jana Jijini Mwanza
Mkutano huo uliwajumuisha viongozi mbalimbali wa TCCIA Taifa wakiwemo  Rais wa chama, Wenyeviti, Makatibu pamoja na Wajumbe.
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TCCIA Taifa uliofanyika jana Jijini Mwanza
Taswira ya Mkutano Mkuu wa TCCIA Taifa uliofanyika jana Jijini Mwanza katika Ukumbi wa Mwanza Hotel.

No comments:

Powered by Blogger.