LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAULI YA MWAKYEMBE BUNGENI MJINI DODOMA YALETA FARAJA KWA WATUMIAJI WA SIMU NCHINI.

Anaezungumza ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Harison Mwakyembe (Picha kutoka Maktaba).
ELISA  ANATORY 0763345064
EMAIL anatoryelisa@gmail.com
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Harison Mwakyembe amesema kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  zimefikia makubaliano  kuhusu kupunguza gharama za huduma za simu za kimataifa ili kuweka mfumo bora wa mawasiliano baina ya nchi hizo.

Mwakyembe aliyasema hayo hii leo bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha makadilio ya mapato ya wizara yake.

Alisema kuwa nchi hizo wanachama zamekubaliana kushushwa kwa gharama hizo na kuwa dola za Kimarekani 0.7 kwa dakika moja kwa watoa huduma, na dola za kimarekani 0.1kwa dakika kwa watumiaji wa kawaida.

Waziri Mwakyembe aliongeza kuwa nchi hizo zimekubaliana pia kuondoa gharama kwa mpokeaji wa simu iliyounganishwa miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo ambapo alibainisha kwawa viwango hivyo vitaanza kutumika kuanzia mwaka wa fedha wa 2015/2016.

Kuhusu  miundombinu ya barabara, Mwakyembe alisema kuwa serikali imekamilisha ujenzi wa daraja la kimataifa la Lusumo lililopo mpakani mwa Tanzania na Rwanda lenye uwezo wa kupitisha magari manne yenye uzito wa tani 54 kila moja tofauti na magari mawili  yaliyokuwa yakipita katika daraja hilo hapo awali na hivyo kusababisha adha kubwa ya usafilishaji.

No comments:

Powered by Blogger.