BVR JIJINI MWANZA KUZUA MAANDAMANO.
Na:Elisa Anatory
Baadhi
ya wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini
Mwanza wametishia kuandamana endapo kama wakazi wote wa Kata hiyo hawatapa
fursa ya kujiandikisha katika zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la
wapiga kura kutokana na kasi ndogo ya zoezi hilo.
Jana wakazi hao walisema kuwa kasi ya uandikishaji inaenda taratibu
kutokana na uchache wa Mashine za Biometric Voters Regstratin BVR pamoja na mashine hizo kupata hitirafu za
mara kwa mara na hivyo kusababisha watu wengi kukaa katika foleni muda mrefu
wakisubiri kuandikishwa.
Mwenyekiti wa mtaa wa
Buhongwa Magaribi Emanuel Mongo alisema kuwa juzi kulikuwa msururu wa watuzaidi
ya 400 ila walioandikishwa ni watu 50 pekee ambapo jana kulikuwa na msururu wa
watu zaidi ya 700 lakini hadi kufikia majira ya saa sita na nusu mchana watu
takribani 60 ndio walikuwa wameandikishwa.
Kumekuwepo na Ushirikiano hafifu kati ya wasimamizi wakuu wa zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura Jijini Mwanza, kwani licha ya kufuatwa mara kwa mara na wanahabari ili kujibu kero na malalamiko ya wananchi dhidi ya zoezi hilo, wamekuwa hawaonyeshi ushirikiano wowote zaidi ya kusema zoezi linakwenda vizuri.
Pamoja na Wilaya nyingine katika Mkoa wa Mwanza, zoezi la
Uandikishaji Jijini Mwanza (Wilaya ya Nyamagana) lilianza June 09 katika Kata
tano ambazo ni Rwanima, Mkuyuni, Buhongwa, Luchelele pamoja na Mkolani ambapo
zoezi hilo linatarajia kukamilika june 15 mwaka huu na kuendelea katika Kata
nyingine.
No comments: