LIVE STREAM ADS

Header Ads

DHANA POTOFU YASABABISHA WANANCHI KUTOTUMIA DARAJA LA MABATINI JIJINI MWANZA.

Na:George GB Pazzo
Licha ya Uwepo wa daraja la juu kwa ajili ya watembea kwa Miguu katika eneo la Mabatini Jijini Mwanza, bado wamekuwa wakisuasua kulitumia daraja hilo na hivyo kuhatarisha maisha yao kutokana na ajali za vyombo vya moto katika eneo hilo.

Wakizungumza na Radio Metro kupitia Kampeni yake ya Kata kwa Kata, Mtaa kwa Mtaa, baadhi ya waendesha pikipiki katika eneo hilo walisema kuwa wananchi wamekuwa hawatumii daraja hilo kutokana na dhana potofu kwamba kuna mzunguko mrefu katika daraja hilo.

Walisema kuwa kutokana na dhana hiyo potofu, kumekuwa na ajali za mara kwa mara katika eneo hilo ambapo watembea kwa miguu wamekuwa wakigongwa na vyombo vya moto pindi wanapokuwa wakijaribu kuvuka barabara bila kutumia daraja lililopo eneo hilo.

Baadhi ya watumiaji wa daraja hilo walisema kuwa hakuna mzunguko mrefu katika daraja hilo kama inavyoelezwa na baadhi ya wananchi ambapo wamependekeza kuwa itungwe sheria itakazowabana wale ambao hawazingatii matumizi ya daraja hilo.


Daraja la Mabatini lilijengwa na Kampuni ya Nordic Construction Limited ya Tanzania kwa gharama ya shilingi Milioni 899.025 kwa lengo la kupunguza kero ya msongamano wa magari na ajali za mara kwa mara za watembea kwa miguu kugongwa na vyombo vya moto katika eneo hilo la Mabatini, lakini baadhi ya wananchi wamekuwa hawaoni umuhimu wa kulitumia jambo ambalo linahatarisha zaidi maisha yao kutokana na hatari ya kugongwa na vyombo vya moto vinavyopita kwa kasi katika eneo hilo.
                                            Credit:Radio Metro

No comments:

Powered by Blogger.