DIWANI KATA YA MBUGANI JIJINI MWANZA AWAJIA JUU WANAOTANGAZA NIA YA KUGOMBEA KATIKA KATA HIYO.
Diwani wa Kata ya Mbugani Jijini Mwanza Hassan Kijuu (Kulia) akibonga na GB Pazzo (Kushoto).
Na:George GB Pazzo
Diwani wa Kata ya Mbugani Jijini
Mwanza (Chadema) Hassan Hashim Kijuu ameelezea kuwashangaa baadhi ya wanachama
wa chama chake wanaojitokeza na kutangaza nia ya kugombea katika Kata hiyo
wakati bado yuko madarakani.
Kijuu alitoa
Kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza na Mtandao huu ambapo alibainisha kwamba,
kwa mjibu wa kanuni za chama chake (Chadema), mtangaza nia hapaswi kutangaza
kugombea ili hali ukomo wa kiongozi alie madarakani bado haujafikia mwisho.
Kijuu
alisema kuwa anashangazwa na Chama chake kukaa kimya wakati kanuni zinaendelea
kuvunjwa kutokana na maadhi ya makada katika Kata ya Mbugani kutangaza nia ya
kugombea udiwani huku yeye akiwa bado madarakani.
Alisema kuwa
kanuni za chama zinaeleza wazi kuwa yeyote atakaetangaza nia ya kugombea wakati
nafasi ya uongozi anayoitaka bado inashikiliwa na kiongozi alie madarakani, mtu
huyo ni sharti fomu yake izuiliwe ili asiweze kugombea.
Aidha
alisema kuwa hana shaka na nafasi yake ya udiwani kwa kuwa diwani wa Kata ya
Mbugani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu anamjua Mungu hivyo hana wasiwasi na
wote waliotangaza nia ya kugombea katika Kata hiyo.
Tayari
Makada kadhaa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika Kata ya
Mbugani wametangaza nia ya Kugombea udiwani katika Kata hiyo, ambapo miongoni
mwa makada hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Unguja Richard Daniel Kajuna.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
No comments: