KATIBU WA CCM TAIFA ABDULRAHMAN KINANA KUUNGURUMA MKOANI MWANZA.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (katikati meza kuu) akizungumza na Wanahabari hii leo.
Na:George GB Pazzo
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi
CCM Taifa Abdulrahman Kinana anatarajia kufanya ziara ya Siku Kumi katika Mkoa
wa Mwanza, ambapo pamoja na mambo mengine anatarajia kukagua utekelezaji wa
Ilani ya chama hicho pamoja na kuwahutubia wananchi kupitia Mikutano ya
hadhara.
Katibu wa
Chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu aliyasema hayo hii leo ofisini kwake,
wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na ziara hiyo.
Mtaturu
alisema kuwa Kinana anatarajiwa kupokelewa June 21 katika Wilaya ya Sengerema
akitokea Mkoani Geita ambapo ataanza rasmi ziara yake ya siku mbili Wilaya humo
kabla ya kuendelea katika Wilaya nyingine za Mkoa wa Mwanza.
“June 21 na
22 atakuwa Wilaya ya Sengerema, June 23 atakuwa Wilaya ya Misungwi, June 24 na
25 atakuwa Wilaya ya Kwimba, June 26 atakuwa Wilaya ya Magu, June 27 atakuwa
Wilaya ya Nyamagana, June 28 atakuwa katika Wilaya ya Ilemela ambapo pia
atawahutubia wananchi katika Uwanja wa Furahisha, June 29 na 30 atakuwa Wilaya
ya Ukerewe”. Alisema Mtaturu.
Mtaturu aliwahimiza
wananchi kujitokeza kwa wingi katika Mikutano yote ya Kinana ukiwemo Mkutano wa
hadhara wa Nyamagana na Ilemela utakaofanyika jumapili ijayo June 28 katika
uwanja wa Furahisha kuanzia majira ya saa tisa mchana.
Kutoka Kushoto ni Issack Kalleiya ambae ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza akifuatiwa na Miraji Mtaturu ambae ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza na Wa wisho ni Loth Olelemeirut ambae ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela.
Wanahabari
Wanahabari
Wanahabari
No comments: