LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA WAZIDI KUMKUBALI MSANII BLACK D BAADA YA KUACHIA NEW HIT SONG NYINGINE.

"MSANII BLACK D"
 Na:Binagi Media Group
Baada ya kutesa na ngoma mbili alizoziachia awali ambazo ni VITA NA NJAA pamoja na NIMETAMBUA, hatimae msanii BLACK D kutoka Mkoani Mara ambae kwa sasa anafanya Mishe zake za Muziki katika ardhi ya Miamba ya Rock City Mwanza-Mwanza ameachia HIT SONG nyingine inayokwenda kwa jina la BADO NIKO NAWE.

Bado niko nawe ni Hit song ambayo imesukwa na Producer Hamis Kamanda kutoka Studio za HashBase Records huku mwimbaji mwenye sauti ya kuwapagawisha mabebezi T-Nock akipewa shavu ndani yake.

"Kiukweli Mwanza Wananikubali sana na nawashukuru kwa namna walivyonipokea vyema kuanzia ngoma yangu ya kwanza hadi hii ya Bado Niko Nawe hivyo nawaahidi kuwa nitaendelea kukaza zaidi kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanapata kitu roho inapenda". Alisema Msanii Black D ambae bado yuko katika majonzi makubwa baada ya kumpoteza meneja wake ambae alifariki hivi majuzi.
Sikiliza na Pakua Ngoma hiyo HAPA

Wa kwanza Kushoto ni Msanii Black D akiwa na Mastaa wengine wanaochipukia kutoka Rock City.

No comments:

Powered by Blogger.