DIWANI WA KATA YA MBUGANI JIJINI MWANZA AELEZA MENGI KABLA YA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA.
Kushoto ni GB Pazzo ambae ni C.E.O wa Mtandao huu na Mtangazaji/ Mwandishi Radio Metro akizungumza na Diwani wa Kata ya Mbugani Jijini Mwanza (Chadema) Hassa Hashim Kijuu (Kulia).
Na:George GB Pazzo
Diwani wa Kata ya Mbugani (Chadema) Jijini
Mwanza Hassan Kijuu amesema kuwa katika kipindi cha Miaka Mitano ya Uongozi
wake unaoelekea Ukingoni, ameweza kuibadili Kata hiyo kimaendelea katika sekta
mbalimbali.
Kijuu alitoa Kauli hiyo jana wakati
akizungumza na Radio Metro kupitia Kampeni ya Mtaa kwa Mtaa, kuhusu namna
alivyosimamia shughuli za Maendeleo katika uongozi.
Alisema kuwa wakati anaingia
madarakani mwaka 2010, Kata ya Mbugani ilikuwa ilikuwa inakabiliwa na changamoto
nyingi za kimaendeleo ambapo asilimia kubwa ya changamoto hizo zimekwisha
tatuliwa huku chache zilizobaki zikiwa katika Mikakati ya kutafutiwa ufumbuzi.
Alizitaja baadhi ya Changamoto hizo
kuwa ni pamoja na kuboresha sekta ya Elimu, Maji, Umeme, Ujenzi wa Vivuko
katika Mto Mirongo, huku akifafanua kuwa changamoto za Mafuriko katika eneo la
Mabatini pamoja na ukarabati wa baadhi ya miundombinu ya barabara katika Kata
hiyo bado zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi.
Kijuu alibainisha kuwa amesimamia vyema
suala la ujenzi wa Vyoo bora katika shule zote tisa za Msingi katika Kata ya
Mbugani ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa shule hizo zinaondokana na tatizo
la Upungufu wa Madawati uliokuwa ukizikabili hapo awali.
Katika hatua nyingine Kijuu
alitanabaisha kwamba anatarajia kutetea nafasi yake ya uongozi baada ya kupokea maombi
kutoka kwa wakazi wa Kata ya Mbugani ambao wamemuomba achukue fomu ya kugombea udiwani
katika Kata hiyo kwa lengo la kuendelea kuwatumikia katika awamu nyingine ya
uongozi ijayo.
Kushoto ni Alphonce Tonny Kapela ambae ni Mtangazaji na Mkuu wa Vipindi Radio Metro akizungumza na Diwani wa Kata ya Mbugani Jijini Mwanza (Chadema) Hassa Hashim Kijuu (Kulia).
Kushoto ni Alphonce Tonny Kapela ambae ni Mtangazaji na Mkuu wa Vipindi Radio Metro akizungumza na Diwani wa Kata ya Mbugani Jijini Mwanza (Chadema) Hassa Hashim Kijuu (Kulia).
Credit:Radio Metro
No comments: