LIVE STREAM ADS

Header Ads

HII NDIYO KAULI YA KITWANGA KUHUSIANA NA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI NCHINI.

Baadhi ya Wanafunzi wenye Ulemavu wa ngozi wanaosoma katika Shule ya Msingi Mitindo ilipo Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza. Shule hiyo inatoa elimu kwa Wanafunzi wa Elimu Maalumu kama vile Ualibino, Uoni hafifu pamoja wasiosikia.
Na:George GB Pazzo
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga amesema kuwa Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za Kisheria wale wote wanaojihusisha na Vitendo vya Ukatili na Mauaji kwa Watu wenye Ulemavu wa ngozi nchini.

Kitwanga ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mkoani Mwanza alitoa kauli hiyo jana, wakati akikabidhi Msaada wa Vifaa vya Umeme wa Jua Sola vilivyotolewa na Kampuni ya Mobisol katika Shule ya Msingi Mitindo iliyopo jimboni humo ambayo inatoa elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji ya elimu maalumu.

Kitwanga alisema kuwa mtu yeyote atakaebainika kujihusisha na vitendo hivyo sheria kali zitachukuliwa dhidi yake, kwa kuwa vinalitia aibu kubwa taifa licha ya kuwa havikubaliki katika jamii.

Aidha Kitwanga aliwaomba Wananchi kujiepusha na vitendo vya Imani za kishirikina ambavyo vimekuwa vikitajwa kusababisha kukithiri kwa vitendo vya ukatili na Mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa minajiri ya kupata utajiri na kupandishwa vyeo.

Mkuu wa Shule ya Msingi Mitindo Mwalimu Kulwa Justo Ng’hwelo aliishukuru Kampuni ya Mobisol kwa msaada wa Sola ilioutoa katika shuke hiyo ambapo ameongeza kuwa jamii inapaswa kuendelee kuelimishwa ili kuondokana na imani za kishirikina, jambo ambalo litasaidia kuondokana na vitendo vya ukatili na mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.

Nae Alfred Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ulemavu Mkoani Mwanza, alisema kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo wadau mbalimbali wanapaswa kujitokeza kwa lengo la kuwasaidia kama ambavyo Kampuni ya Mobsol ilivyofanya.

Kwa upande wake Robert Sanyagi ambae ni Meneja wa Kampuni ya Mobsol Kanda ya Ziwa alisema kuwa kampuni hiyo imeamua kutoa vifaa hivyo vya nishati ya umeme wa jua katika shule hiyo ya Mitindo kwa lengo la kusaidia kuondoa changamoto iliyokuwepo  katika shuleni hapo pindi Umeme wa Tanesco ulipokuwa ukikatika.


Kampuni ya Mobsol ambayo ni watengenezaji wa Vifaa vya Kufua nishati ya Umeme wa Jua Sola, ilitoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni tatu na laki sita katika Shule hiyo ya Msingi Mitindo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga akikabidhi mitambo mitano ya kufua umeme wa jua katika Shule ya Msingi Mitindo iliyopo Misungwi. Mitambo hiyo imetolewa na Kampuni ya Mobsol
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga akiangalia mtambo wa kufua umeme wa jua
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga akipokea maelezo juu ya mitambo ya kufua umeme wa jua ya Mobsol
Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga akizungumza wakati wa kukabidhi mitambo ya kufua umeme wa jua iliyotolewa na Kampuni ya Mobsol
Aliesimama ni Elius Nyakia ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kufua umeme vya Mobsol
Aliesimama ni Kulwa Justo Ng'hwelo ambae ni Mkuu wa Shule Mitindi, akifuatiwa na Kalunde Kushaba ambae ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, akifuatiwa na Alfred Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ulemavu Mkoani Mwanza, anaefuata ni Emmanuel Aligaivesa ambae ni Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Misungwi, akifuatiwa na Elius Nyakia ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi na wa mwisho ni Elius Nyakia ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi.
Meza Kuu.
Kutoka kulia ni Samuel Schuster ambae ni Meneja Miraji kutoka Kampuni ya Mobsol, akifuatiwa na Robert Sanyagi ambae ni Meneja wa Kampuni hiyo, anaefuata ni Elius Nyakia ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi na wa Mwisho ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga
Robert Sanyagi (Kushoto) ambae ni Meneja wa Kampuni ya MOBSOL Kanda ya Ziwa akizungumza na wanahabari.
Waliosimama ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya MOBSOL
PICHA YA PAMOJA

No comments:

Powered by Blogger.