LIVE STREAM ADS

Header Ads

TFDA YAFUNGA KIWANDA CHA TRUE BEATY LIMITED KWA KUZALISHA BIDHAA BILA USAJILI.

Hii leo Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA imekifungia Kiwanda cha TRUE BEATY LIMITED kilichopo Kitangiri Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa kosa la kuzalisha bidhaa za chakula huku kikiwa hakijasajiliwa na Mamlaka hiyo.
Na:Tumeinyaka Kupitia Whatsupp
Pichani ni baadhi ya bidhaa zilizokamatwa katika kiwanda hicho ambacho ni mali ya Gelard Bwana. Kiwanda hicho kilikuwa kikizalisha bidhaa mbalimbali za chakula ambazo ni pamoja na Juice ya Matunda (kama vile embe, nanasi na chungwa) pamoja na Thomato Sauce huku kikiwa hakijasajiliwa na Mamlaka hiyo. Yalipo makazi ya mmiliki wa Kiwanda hicho ndipo kilipokuwa kiwanda.
Nuru Mwasulama ambae ni Mkaguzi wa Chakula kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Kanda ya Ziwa akizungumza na wanahabari
Kulia ni Gelard Bwana ambae ni Mmiliki wa Kiwanda cha True Beaty Limited ambapo amefikishwa rumande yeye pamoja na bidhaa zake bila kusahau mitambo yake ya uzalishaji.
Afisa Kutoka TFDA akifunga Kiwanda cha True Beaty Limited kilichopo Kitangiri Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, kilichokuwa kikizalisha bidhaa bila usajili wa Mamlaka hiyo.
Binagi Media Group-0757 43 26 94 kwa tukio lolote

No comments:

Powered by Blogger.