LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI WA KATA JIRANI WAVAMIA KATA YA MKOLANI JIJINI MWANZA ILI KUJIANDIKISHA.

Na:Elisa Anatory
Zoezi la wananchi Kujiandikishwa katika daftari la wapiga kura katika Kata ya Mkolani limeshindwa kukamilika kwa wakati, kutokana na baadhi ya wananchi kutoka nje ya Kata hiyo kufika kwa ajili ya kuandikishwa Katani hapo.

Hayo yalielezwa jana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkolani hiyo Godfrey Mwangomba alisema kuwa watu wamekuwa wakitoka katika maeneo jirani na kata hiyo na kwenda kujiandikisha katika yake jambo ambalo limesababisha mashine za Biometric Voters Registration BVR zilizopo Katani hapo kuzidiwa na ongezeko la idadi ya wananchi.

Aidha Mwangomba aliongeza kuwa zoezi hilo lililoanza tangu June 09 mwezi huu hadi sasa wananchi walioandikishwa ni zaidi ya Elfu Kumi huku akishindwa kubainisha Kata hiyo ina wakazi wangapi wenye sifa ya kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.

Zoezi la Uandikishaji katika Kata ya Mkolani lilitarajiwa kufikia tamati jana June 15, lakini lakini haikuwa hivyo kutokana na idadi kuwa ya wananchi iliyokuwa bado haijaandikishwa hali ambayo iliilazimu Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nec kuongeza siku moja ambayo ni leo ya zoezi hilo kuendelea.

Nao baadhi ya wakazi wa Kata hiyo walisema kuwa kwa muda wa siku moja ambao NEC imeuongeza kwa ajili ya uandikishaji Katani hapo bado hautoshi kwa kuwa bado kuna idadi kubwa ya wananchi ambao hawajapata fursa ya kuandikishwa.

No comments:

Powered by Blogger.