TOTO AFRICAN YA JIJINI MWANZA KUTUMIA SHILINGI MILIONI 495 KATIKA MSIMU UJAO WA LIGI KUU.
N:Oscar Mihayo
Klabu ya Toto African ya Jijini Mwanza imetenga kiasi cha Sh.495 Milioni kwa ajili
ya Bajeti ya msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikiwa ni moja ya mipango
yake ya kuhakikisha inafanya vizuri na kuwa tishio ya vigogo wa ligi hiyo.
Akizungumza
kwenye mkutano mkuu wa Klabu hiyo uliofanyika juzi Jijini Mwanza, Makamu
Mwenyekiti wa timu hiyo Ahmed Waziri Gao alisema kuwa kutokana na ushindani
uliopo kwa vilabu vya ligi kuu, kamati tendaji ya timu hiyo imetenga kiasi
hicho cha fedha ambacho kitaweza kutumika kwa ajili ya msimu ujao.
“Kuna ugumu
na ushindani wa ligi kuu kwani vilabu vimejipanga Kwa hiyo na sisi kama kamati
tendaji tumepanga kutumia kiasi cha Sh.495 ambacho kitaweza kutumika kwenye
msimu ujao lengo likiwa ni kutusaidia kupata ubingwa na si kushiriki tu”. Alisema
Gao.
Bajeti hiyo
iliungwa mkono na wanachama waliohudhuria mkutano huo ambapo walisema kuwa huu
ni muda muafaka wa maandalizi ya Klabu hiyo, hivyo bajeti hiyo itasaidia kuinua
timu yao.
Akifafanua
matumizi ya fedha hizo Katibu Mkuu wa Klabu hiyo Ernest Shija Mpiwa alisema
kuwa Usajili utagharimu kiasi cha shilingi Milioni 30,Mishahara milioni 138 na
Safari milioni 40.
Nyingine ni
Kambi shilingi milioni 165, Uhamisho Milioni sita, Vifaa tiba milioni mbili huku
Uendeshaji wa timu hiyo pamoja na ile ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 zikitengwa
shilingi Milioni 145.
Katibu huyo
alisema kuwa bajeti hiyo itasaidia kubadilisha hali ya Klabu na mazingira kwa ujumla
na hivyo kuweza kuifanya timu ya Toto kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi.
“Hii bajeti
tuna matumaini itatuweka katika hali nzuri ikiwa ni pamoja na kubadilisha hali
na mazingira ya Klabu hivyo kupitishwa kwake ni mafanikio kwa timu yetu.”Alisema
Mpiwa.
Aidha mmoja
wa wanachama wa klabu hiyo Kabuka Magalula aliomba kamati ya usajiri kusajili
kujikiza zaidi katika kusajili wachezaji wazawa na kuachana na wachezaji
walioachwa na timu kubwa kama Simba na Yanga kwani huo utakuwa ndio mwisho wa
hujuma za wacheza kutoka klabu hizo kubwa hapa nchini.
No comments: