LIVE STREAM ADS

Header Ads

LICHA YA KUKOSA TUZO ZA KILI, CHRISTIAN BELLA APOKELEWA VYEMA MKOANI TABORA.

Christian Bella akijimwaga jukwaani Onesho lililofafanyika katika viwanja vya Bwalo la Polisi Tabora.
Picha na habari :Mkala Fundikira TBN CENTRAL ZONE
Masaa machache baada ya kukosa kitatanishi tunzo ya wimbo bora wa mwaka katika Kili Music Awards Christian Bela (King of melodies) Juzi jumapili alipagawisha wapenzi wa muziki mjini Tabora alipoporomosha bonge la show akiwa na kundi zima la Malaika Band. 

Christian Bela alitarajiwa na  wadau wa muziki nchini kuwa angebeba tuzo hiyo bila ushindani mkubwa kutokana na wimbo wake wa Nani kama mama ambao aliomshirikisha Ommy Dimpoz kutamba sana katika vituo vyote vya redio na Runinga hapa nchini.

Lakini kama kawaida ya tuzo hizo zinazosimamiwa na BASATA na kudhaminiwa na kampuni ya utengenezaji bia ya Tanzania TBL zimekuwa zikilalamikiwa kila mwaka huku waanadaaji wakioneka kuweka pamba mbichi masikioni. Tuzo hiyo ya wimbo bora wa mwaka ilienda kwa wimbo wa Mwana wa msanii Ali Kiba
Bella akifanya yake jukwaani.
Mashabiki wa Malaika Band wakpozi
Hapo sasa!
Show hatareeeeee
Baadhi ya mashabiki wakijmwaga!
Mashabiki
Bella kwa Stage
Music Producer Dula K kulia na msanii Masha Kay kushoto wakiwa na mdau.
Mashabiki wa Bella
Wacha wee Benny Ngwasuma akijiachia
Bella akinogisha Kwa Jukwaa Mkoani Tabora

No comments:

Powered by Blogger.