LIVE STREAM ADS

Header Ads

MABIBI NA MABWANA NAMLETA KWENU MSANII STAFFA BAADA YA KUACHIA WIMBO WAKE MPYA.

MSANII STAFFA KUTOKA MWANZA.
Na:George GB Pazzo
Mabibi na Mabwana, Kwa Heshima na Taadhima, kama ilivyo ada ya BINAGI MEDIA GROUP; Kwa Pamoja Tuijuze Jamii, huwa inakusogezea karibu ngoma mpya kutoka kwa Wasanii wa Kanda ya Ziwa hivyo tunayo Furaha tele pia kwa siku ya leo kumleta kwenu Msanii Mustafa Omary a.k.a Staffa Kutoka Igombe Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.

Huyo ni Mmoja wa Wasanii chipukizi wanaokuja vizuri kwa Mwaka huu 2015 ambapo Msanii huyu ameachia ngoma yake ya kwanza ambayo inakwenda kwa jina la "NINUSURU" ikiwa katika mahadhi ya Kubana pua ambapo goma hiyo imetengenezewa katika Studio ya Rock Town Records ikiwa ni kampani kutoka kwa mshikaji wake ambae kwa sasa anammeneji.
SIKILIZA HAPA CHINI NGOMA YAKE STAFFA-NINUSURU.

NAFTARY MATIAS AMBAE NI MENEJA WA MSANII MUSTAFA OMARY a.k.a STAFFA.
MSANII MUSTAFA OMARY a.k.a STAFFA KUTOKA MWANZA (KULIA) AKIWA NA MENEJA WAKE NAFTARY MATIAS.
SOURCE:BINAGI MEDIA GROUP

No comments:

Powered by Blogger.